James Cook

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
James Cook mnamo 1775 (picha na Nathaniel Dance

James Cook (tamka: jems kuk * 27 Oktoba 1728 Uingereza, † 14 Februari 1779 Hawaiʻi) alikuwa nahodha na mpelelezi Mwingereza katika karne ya 18.

Amejulikana hasa kutokana safari tatu katika Bahari ya Pasifiki na taarifa zake juu ya safari hizi. Cook alitembelea visiwa vingi visivyojulikana Ulaya hadi wakati ule akivipima na kuvichora kwa ramani.

Alizunguka dunia yote mara mbili. Kati ya maeneo aliyoyaweka kwenye ramani za dunia ni pwani la mashariki ya Australia, visiwa vya Hawaii, Newfoundland na New Zealand.

Cook aliuawa na wenyeji wa Hawaii alipotembelea kisiwa mara ya tatu.

Visiwa vya Cook hutunza kumbukumbu ya jina lake.