Wamaori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Te Puni, chifu wa Wamaori wa karne ya 19.

Wamaori ni wakazi asilia wa New Zealand. Walikuwa ndio watu wa kwanza kufika kwenye visiwa hivyo.

Mababu zao walikuwa watu wa Polynesia waliofika New Zealand kati ya mwaka 800 na 1300 BK. Katika mapokeo ya Wamaori, mahali wanakotokea huitwa Hawai'iki ila haijulikani iko wapi. Hivyo hakuna uhakika walipotokea, maana wataalamu wanajadiliana kwa kutaja Visiwa vya Cook au visiwa vilivyopo sasa Polynesia ya Kifaransa kama Tahiti.

Katika lugha yao, "Maori" inamaanisha "kawaida". Waliwaita watu wengine, haswa wale waliokuja kutoka Uingereza, "Pākehā". Leo katika Kiingereza cha New Zealand "Pākehā" hutumiwa mara nyingi kama jina la Wazungu wa New Zealand.

Leo wako takriban Wamaori 600,000 wanaoishi New Zealand. Wao ni sehemu muhimu ya utamaduni wa nchi. Hii ndiyo sababu ya kwamba wamepokea haki maalum kutoka kwa serikali ya New Zealand. Lugha yao ya asili, lugha ya Kimaori, ni lugha rasmi ya nchi hiyo pamoja na Kiingereza.

Tovuti za nje[hariri | hariri chanzo]