Guyani ya Kifaransa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Guyana ya Kifaransa)
Guyane
Lagwiyann
Nembo
Jina la Kifaransa Guyane
(kwa Krioli:Lagwiyann)
Jina la kawaida Guyani ya Kifaransa
Mji Mkuu Kayeni
Eneo 86 504 km²
Mkuu wa Mkoa Gabriel Serville
Idadi ya wakazi 301 099
Sensa ya mwaka 2022
Wakazi kwa km² 3.2
Wilaya (arrondissements) 3
Ramani
-- Kwa nchi jirani angalia makala Guyana--

Guyani ya Kifaransa (kwa Kifaransa: Guyane française au Guyane tu, kwa Krioli ya Guyani ya Kifaransa Lagwiyann) ni eneo la ng'ambo la Ufaransa ("département d'outre-mer" au DOM) katika Amerika Kusini. Makao makuu ya Guyana ni mji wa Kayeni.

Imepakana na Brazil na Surinam. Pwani ya Bahari ya Karibi (Atlantiki) iko upande wa kaskazini.

Eneo la Guyani ni mojawapo ya mikoa tisa ya nje zaidi (OR) ya Umoja wa Ulaya. Ni eneo pekee la bara la Ufaransa na Umoja wa Ulaya huko Amerika Kusini na eneo la mwisho la Ufaransa katika bara la Amerika.

Ilikuwa koloni la Ufaransa; sasa imekuwa sehemu kamili ya Ufaransa kisiasa na kisheria. Wakazi ni raia wa Ufaransa. Eneo lina hali ya mkoa (fr:département) na pia kanda (fr:région) katika Ufaransa. Hivyo Guyani ni sehemu ya Umoja wa Ulaya. Pesa yake ni Euro.

Watu

Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa 296,711 katika mwaka 2019 na inaendelea kuongezeka kwa uzazi na uhamiaji.

Wakazi walio wengi ni wa asili ya Afrika au machotara wa mchanganyiko wa Kiafrika-Kizungu (Wakrioli) (60-70%). Asilimia 14 ni Wazungu, hasa kutoka Ufaransa; wengine ni Waindio asilia (3-4%), Wachina (3-4%), Wahindi na wahamiaji wa hivi karibuni kutoka Laos (1-2%), Vietnam, Lebanoni n.k.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kifaransa.

Upande wa dini, wakazi walio wengi ni Wakristo wa Kanisa Katoliki (66.7%).

Tazama pia

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guyani ya Kifaransa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.