Chile

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chile


Chile ni nchi ya Amerika Kusini.

Eneo lake ni kama kanda ndefu nyembamba kati ya safu za milima ya Andes na Bahari ya Pasifiki.

Imepakana na Peru, Bolivia na Argentina.

Ni sehemu za Chile pia maeneo ya Kisiwa cha Pasaka (Rapa Nui), Kisiwa cha Salas y Gómez, Visiwa vya Juan Fernández (pamoja na kisiwa cha Robinson Crusoe), visiwa vya Desventuradas, Visiwa vya Ildefonso na visiwa vya Diego Ramirez.

Chile inadai ya kuwa sehemu ya bara la Antaktika ni eneo lake.

Ramani ya Chile.

Mji mkuu ni Santiago, yaani Mtakatifu Yakobo.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Chile ina urefu wa kilomita 4,200 kufuata pwani ya Pasifiki na milima ya Andes. Umbali huu ni kama kutoka Cape Town kwenda Dar es Salaam. Lakini upana wa wastani wa eneo lake ni kilomita 180 tu: sehemu nyembamba ya nchi ina upana wa kilomita 90, sehemu pana zaidi ina kilomita 240.

Nje ya maeneo yenye uwanja mwembamba wa pwani, nchi yote ni ya milima na mabonde. Sehemu kubwa ya nchi ina safu mbili za milima:

Katikati ya safu hizo mbili kuna bonde la kati (Valle Central) lenye makazi ya idadi kubwa ya wananchi na ardhi yenye rutuba kwa kilimo.

Kuelekea kusini kimo cha nchi hushuka hadi kufikia chini ya uwiano wa bahari. Milima ya safu ya pwani huonekana sasa kama visiwa.

Kaskazini mwa nchi hakuna bonde kubwa la kati. Nchi inapanda juu kutoka mwambao wa bahari hadi kuwa tambarare yenye kimo cha mita 1,000 - 1,500 inayoendelea mpaka mwanzo wa safu ya Andes.

Milima[hariri | hariri chanzo]

Andes za Chile ni kati ya milima ya juu duniani: kuna vilele kadhaa juu ya mita 6,000.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Atacama.

Wakazi wengi (85%) wanaishi mijini. Utafiti juu ya DNA yao unaonyesha kwa asilimia 52% hivi ina asili ya Ulaya, 43% ni ya Kiindio na 5% ni kutoka Afrika. Kwa jumla, wengi wana mchanganyiko wa damu.

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kihispania.

Upande wa dini, 66.6% ni Wakatoliki na 17% ni Waprotestanti. Asilimia 12.4 haina dini yoyote.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Amerika Kusini

Argentina | Bolivia | Brazil | Chile | Ekuador | Guyana | Guyani ya Kifaransa | Kolombia | Paraguay | Peru | Surinam | Uruguay | Venezuela

Makala hii kuhusu maeneo ya Chile bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chile kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.