Îles Éparses

Îles Éparses (Kifaransa kwa "visiwa vilivyotawanyika") ni atolli na visiwa vidogo katika Bahari ya Hindi vinavyotawaliwa na Ufaransa. Haviko chini ya mkoa wowote au kitengo kingine kati ya maeneo ya ng'ambo ya Ufaransa. Havihesabiwi kama mkoa wa pekee kwa sababu hakuna wakazi asilia isipokuwa watumishi wa serikali, wanajeshi au wanasayansi kwenye vituo mbalimbali visiwani.
Hadi mwaka 2005 vilisimamiwa na mkuu wa mkoa wa Réunion lakini havikuhesabiwa kati ya maeneo ya Umoja wa Ulaya kama Reunion yenyewe. Tangu hapo kuna afisa mtawala mwenye cheo cha mkuu wa mkoa (prefect) kwa ajili ya Îles Éparses pamoja na visiwa katika Bahari ya Kusini.
Visiwa
[hariri | hariri chanzo]Visiwa hivyo hudaiwa na Madagaska na Tromelin inadaiwa na Shelisheli pia.
Mnamo Aprili 2025, Ufaransa na Madagaska zilitangaza kwamba watakutana Juni 2025 kutafuta suluhu ya amani kwa mzozo huo. Mnamo 20 Juni 2025, Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagaska, Rasata Rafaravavitafika, aliongoza mkutano wa kamati ya kisayansi inayohusu madai ya Madagaska kwa Visiwa Vilivyotawanyika. Lengo la mkutano huo lilikuwa kuendeleza hoja za kuhifadhi mamlaka ya Madagaska juu ya Visiwa Vilivyotawanyika, huku wakiendeleza majadiliano na Ufaransa.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya Wizara ya maeneo ya ng'ambo ya Ufaransa Ilihifadhiwa 28 Aprili 2016 kwenye Wayback Machine. (Kifaransa)
- Tovuti rasmi (Kifaransa)
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Îles Éparses kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |