Visiwa vya Virgin vya Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Visiwa vya Virgin vya Marekani

Visiwa vya Virgin vya Marekani (United States Virgin Islands) ni visiwa katika Bahari ya Karibi ambavyo viko chini ya Marekani, wakazi ni raia wa Marekani lakini hawashiriki katika uchaguzi wa Rais wala wa bunge la Washington DC. Viko takriban km 80 upande wa mashariki wa Puerto Rico.

Ni sehemu ya funguvisiwa la Visiwa vya Virgin lililogawiwa kati ya Uingereza na Marekani. Kisiwa cha Saint John cha Marekani ni karibu sana na kisiwa cha Tortola upande wa Uingereza. Pande zote mbili za funguvisiwa kuna ushirikiano wa kiuchumi zikitumia dollar ya Marekani.

Ni hasa visiwa vya St. Thomas, St. John, St. Croix pamoja na visiwa vidogo 50 hivi.

Eneo lao kwa jumla ni km² 346.36. Sensa ya mwaka 2020 ilihesabu wakazi 87,146, ambao kati yao 76% wana asili ya Afrika na 15.7% ya Ulaya.

Karibu wote (94.8%) ni Wakristo, hasa Waprotestanti (65.5%), lakini pia Wakatoliki (27.1%). Lugha kuu ni aina za Kiingereza, halafu za Kihispania na za Kifaransa.

Visiwa hivyo ni sehemu pekee ya Marekani ambako magari yanasafiri upande wa kushoto wa barabara.

Visiwa vilikuwa koloni la Denmark vikauzwa kwa Marekani tarehe 17 Januari 1917 .


Majimbo na maeneo ya Marekani
Majimbo ya Marekani
AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming
Mkoa wa Mji Mkuu
Mkoa wa Columbia (Washington D.C.)
Visiwa vya ng'ambo
Katika Pasifiki: Samoa ya MarekaniVisiwa vya Mariana ya KaskaziniGuamKatika Karibi: Puerto RicoVisiwa vya Virgin vya MarekaniVisiwa vidogo sana vya Pasifiki:Kisiwa cha HowlandKisiwa cha Jarvis Atolli ya JohnstonKingman ReefAtolli ya MidwayKisiwa cha BakerAtolli ya PalmyraKisiwa cha WakeKisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya Virgin vya Marekani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.