Historia ya Uzbekistan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Historia ya Uzbekistan inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Uzbekistan.

Uzbekistan ni nchi yenye historia ndefu. Ferghana, Tashkent, Bukhara, Khwarezm na Samarkand zilikuwa vitovu vya utamaduni wa binadamu tangu milenia ya 2 KK.

Katika karne kabla na baada ya Kristo eneo lilijulikana kama Sogdiana na Baktria. Miji yake ilikuwa na utajiri kutokana na biashara ya misafara kwenye barabara ya hariri kati ya China na Mashariki ya Kati.

Baadaye ilitawaliwa na milki mbalimbali za nje kama Uajemi.

Kuanzia uenezi wa Uislamu watu ba Uzbekistan waligeukia dini hiyo mpya.

Katika karne ya 14 jemadari Timur alijenga milki kubwa na kuharibu nchi za magharibi hadi Uturuki. Alipamba mji mkuu wake Samarkand kwa majengo mazuri.

Baada ya Timur milki yake iliporomoka na Uzbekistan ilitawaliwa na madola mbalimbali ya kieneo yaliyokuwa hasa eneo la mji muhimu.

Katika karne ya 19 Urusi ulieneza athira yake kuelekea kusini na kuunganisha madola ya Uzbekistan na milki yake.

Baada ya mapinduzi ya Urusi ya mwaka 1917 Uzbekistan ikawa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi kusambaratika kwake mwaka 1991. Wakati huo ilijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki".

Tarehe 31 Agosti 1991 ilijitangaza huru na kudai kufuata demokrasia na kuelekea soko huria, lakini hadi sasa haki za binadamu haziheshimiwi sana.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Uzbekistan kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.