Bukhara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Majengo ya kihistoria ya Bukhara

Buckara (Kiuzbeki Buxoro; Kiajemi: بُخارا bukhārā, Kirusi Бухара/Buchara) ni kati ya miji muhimu ya Uzbekistan. Idadi ya wakazi ilikuwa 237,900 (mwaka 1999).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Bukhara ni kati ya miji ya kihistoria iliyostawi tangu miaka elfu mbili mia tano kwenye barabara ya hariri kati ya China na nchi za magharibi. Bukhara ilikuwa hasa sehemu ya milki za Uajemi na kwa muda wa karne mbili mji mkuu wa milki ya Samaniya waliokuwa Wajemi. Tangu mapigano ya Talas mwaka 751 Bukhara pamoja na Asia ya Kati iliingizwa katika himaya ya Uislamu.

Baadaye mji ulikuwa mkononi mwa Wamongolia lakini tabia ya Kiajemi (au kwa lugha nyingine: Kitajiki) ya wakazi wake imebaki hadi leo. Katika karne za 16 na 17 Bukhara ikawa tena mji mkuu wa milki ikapambwa na misikiti, madarasa na majengo mengine mazuri.

Wakati wa upanuzi wa Urusi katika Asia ya Kati dola la Bukhara likawa nchi lindwa chini na jirani mkubwa lakini ilibaki na madaraka kwa ndani hadi kufika kwa jeshi la mapinduzi ya Kibolsheviki katika Uzbekistan mwaka 1920. Bukhara ikatangazwa kuwa jamhuri na 1924 ikaingizwa katika Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiuzbeki na hivyo katika Umoja wa Kisovyeti.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Kuna majengo mazuri ambayo ni sababu ya kuandikishwa kwa Bukhara katika orodha la urithi wa dunia la UNESCO.

Wakazi walio wengi wanatumia lugha ya Kitajiki.


Picha za Bukhara[hariri | hariri chanzo]