Nenda kwa yaliyomo

Nasaba ya Qin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nasaba ya Qin

Nasaba ya Qin (Ch'in) ilikuwa nasaba ya kwanza ya kifalme ya China yote. Ilidumu kuanzia mwaka 221 KK hadi 206 KK. Nasaba hiyo ilikuwa na Makaisari wawili tu: Qin Shih Huangdi, na Qui Er-Shihdi.

Kiasili ufalme wa Qin ulikuwa moja kati ya milki zilizoshindana katika China kaskazini tangu kudhoofishwa kwa nasaba ya Zhou. Qin ilifaulu kushinda falme nyingine hadi mwaka 221 KK. Kwa hiyo Qin ilikuwa nasaba ya kwanza iliyofaulu kuunganisha Wachina wa Wahan wote[1].

Baada ya kuunganisha maeneo hayo mfalme Zheng alikuwa mtawala wa kwanza aliyetumia cheo cha "Huangdi" inayolingana na Kaizari akajulikana kama kwa jina la kikaizari Shih huang-ti.

Aliweka misingi iliyodumu kwa milenia[2]: utawala kupitia watumishi walioajiriwa na milki, sensa ya wakazi na ardhi kwa kupanga kodi, ukuta wa ulinzi dhidi ya makabila ya Asia ya Kati, matumizi ya vipimo, sarafu na mwandiko wa pamoja.

Baada ya kifo cha kaizari wa kwanza milki iliingia katika kipindi cha matatizo na vita ya wenyewe kwa wenyewe. Hatimaye waasi walimwua kaizari wa tatu Ziying kwenye mwaka 207.

Kaizari wa kwanza Qin Shi Huangdi aliacha kaburi lake kubwa karibu na mji wa Xi-an lenye sanamu elfu nyingi za wanajeshi zinazojulikana kama jeshi la terakota.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Derk Bodde: The state and empire of Ch'in. In: The Cambridge History of China. Band 1: The Ch'in and Han Empires, 221 B.C. – A.D. 220. 1986, S. 20–102, hier S. 69.
  2. Mary B. Rankin, John K. Fairbank, Albert Feuerwerker: Perspectives on modern China's history. In: The Cambridge History of China. Band 13: Republican China 1912–1949. Part 2. Cambridge University Press, Cambridge u. a. 1986, ISBN 0-521-24338-6, S. 1–73, hier S. 49.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nasaba ya Qin kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.