Mauti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Fuvu la kichwa, ishara maarufu ya kifo.
Idadi ya vifo kati ya watu milioni moja mwaka 2012
     1054-4,598     4,599-5,516     5,517-6,289     6,290-6,835     6,836-7,916     7,917-8,728     8,729-9,404     9,405-10,433     10,434-12,233     12,234-17,141

Mauti (kutoka Kiarabu موت, maut) au kifo (kutoka kitenzi cha Kibantu kufa) ni mwisho wa uhai; kwa lugha ya biolojia mwisho wa michakato yote ndani ya kiumbehai ambayo ni dalili za uhai.

Chanzo[hariri | hariri chanzo]

Mauti hutokea kutokana na sababu mbalimbali kama vile

  • umri mkubwa unaosababisha michakato ya kimsingi mwilini kusimama polepole
  • muda mrefu wa maisha unaoruhusu makosa na kasoro kujumuika na kusababisha madhara (mfano: kansa)
  • magonjwa yanayovuruga michakato ya uhai hadi kuisimamisha
  • ajali zinazoharibu viungo muhimu mwilini
  • ukosefu wa chakula, maji, hewa au kinga dhidi ya mazingira magumu
  • athari haribifu kutoka viumbe wengine (k.m. kushambuliwa) au kutoka mazingira

Hakikisho[hariri | hariri chanzo]

Kwa binadamu kutokea kwa kifo mara nyingi hakutokei mara moja; katika mazingira ya kawaida kifo kinaonekana kama moyo hausikiki tena na mapafu hayakupumua kwa dakika kadhaa.

Hata hivyo kuna uwezekano wa kwamba kazi ya moyo na mapafu ni hafifu kiasi kwamba haitambuliki. Penye hospitali nzuri na mitambo ya kiganga mara nyingi mtu anarudi kuishi ingawa mahali pengine ametazamwa ameshaaga dunia. Kama mashine zinaendelea kuchukua kazi ya moyo na mapafu si rahisi kujua kifo kinatokea lini.

Wataalamu wengi siku hizi wanapoona michakato ya kawaida ya ubongo imekwisha kwa muda fulani, wanasema kifo kimetokea. Hata hivyo kuna kesi za watu wanaozinduka baada ya muda huo.

Mauti na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Katika utamaduni na imani za watu mauti ni jambo muhimu. Lugha ina njia nyingi za kuitaja kwa mfano kuaga dunia, kufariki dunia n.k.

Katika dini na falsafa kuna misimamo mbalimbali kuhusu mauti kama vile

  1. Mauti ni mwisho wa binadamu kimwili na kiroho; hakuna kinachobaki baada ya kifo
  2. Mauti ni hatua tu katika mzunguko wa maisha; nafsi au roho inarudi katika maumbile mengine
  3. Kifo ni kupita penginepo: uzima wa milele, mbinguni, upeo wa wafu n.k.
Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mauti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.