Nenda kwa yaliyomo

Dola la Ghana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dola la Ghana

Dola la Ghana lilikuwa dola katika eneo la Mali ya leo pamoja na nchi jirani lililotawala upande wa kusini wa njia za Biashara ya ng'ambo ya Sahara.

Dola hilo lilistawi tangu karne ya 2 BK hadi mwaka 1076, likitawala biashara ya dhahabu, pembe za ndovu na chumvi.

Mji mkuu ulikuwa Kumbi Sale wenye wakazi 30,000 katika Mauretania ya leo.

Taarifa za wanahistoria Waarabu zimeonyesha ufalme tajiri.

Utamaduni wake haukuwa wa Kiislamu bali wa Kiafrika asilia.

Mwisho wake ulianza wakati jeshi la Wamurabitun kutoka Moroko lilivuka jangwa la Sahara na kuvamia Kumbi Sale.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dola la Ghana kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.