Milki ya Wamongolia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upanuzi wa Milki ya Mongolia

Milki ya Wamongolia ilikuwa eneo lililotawaliwa na (khans) wa Mongolia kuu kunako karne ya 13 na 14. Hili lilikuwa moja kati ya milki kubwa sana katika historia ya umiliki wa ardhi.

Uenezi[hariri | hariri chanzo]

Nyumbani halisi kwa Wamongolia, ilikuwa imepakana na Milima ya Khingan kwa upande wa mashariki, Milima Altai na Tian kwa upande wa magharibi, Mto Shilka na safu za milima na [Ziwa Baikal]] kwa upande wa kaskazini, na Ukuta Mkubwa wa China kwa upande wa kusini.

Milki hii ilianzishwa na Genghis Khan mnamo 1207 BK pale alipoyaleta pamoja makabila ya Mongolia. Akaja kufa mnamo 1227 BK. Baadaye Kublai Khan akaendeleza kupanua milki hii akakuta Nasaba ya Yuan iliotawaliwa na Wamongolia huko China. Baadaye ikaja kupagalanyika katika milki tofauti, na zote katika hizo ziliangamizwa.

Wakati nguvu ya milki za Wamongolia ilikuwa imepungua tayari, Tamerlan (Timur), aliyetoka katika ukoo wa Kimongolia uliopokea Uislamu, aliunda milki mpya kati ya Uhindi ya magharibi, Asia ya Kati na Syria ya mashariki.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Milki ya Wamongolia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.