Umedi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Eneo la Umedi katika Uajemi ya magharibi
Milki ya kimedi mnamo mwaka 600 KK
Askari ya Kimedi (kushoto) na Mwajemi (kulia); kutoka jumba la kifalme cha Apadana

Umedi ilikuwa nchi na milki ya kihistoria na sehemu kubwa ya eneo lake lilikuwa ndani ya Uajemi ya magharibi ya leo.

Kiasili ni jina linalojumlisha makabila mbalimbali yaliyofika katika Iran ya leo mnamo mwaka 2500 KK. Mnamo mwaka 600 KK Wafalme wa Umedi waliweza kupanua milki yao na kutawala sehemu kubwa za Mashariki ya Kati. Mwaka 539 KK milki yao ilitwaliwa na Koreshi Mkuu na kuendelea kama sehemu ya milki ya Uajemi.

Wafalme wakuu wa Uajemi waliendelea kama "wafalme wa Waajemi na Wamedi" na hivyo jina la Umedi na Wamedi linapatikana mara kadkhaa katika maandiko ya Biblia ya Kiebrania.

Lugha ya Kimedi[hariri | hariri chanzo]

Mwanahistoria Strabo wa Ugiriki ya Kale alisema ya kwamba Kimedi na lugha nyingine za Kiajemi zinafanana.

"Jina la Ariana linataja maeneo zaidi kuliko Uajemi na Umedi, lakini pia Baktria na Sogdia upande wa kaskazini; maana hao wote huzungumza takriban lugha moja ingawa kuna tofauti ndogo za kieneo."[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Strabo, Jiografia 15.8
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Umedi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.