Usultani wa Adal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo yaloharibiwa ya Mfalme wa Adal katika Zeila, Somalia.

Usultani wa Adal (Kisomali: Adaal, Kige'ez: አዳል ʾAdāl, Kiarabu: عدل; c. 1415 - 1555) ulikuwa ufalme wa iliyo sasa Kaskazini-Magharibi ya Somalia, Kusini mwa Jibuti, Somali, Oromia, na Afar iliyo mikoa ya Ethiopia. Katika kipindi cha juu cha uongozi wake, Sultani aliweza kuongoza sehemu kubwa ya eneo la Ethiopia na Somalia.

Makabila[hariri | hariri chanzo]

Bado kuna majadiliano kuhusu asili na idadi ya makabila katika ufalme huu. I.M Lewis anasema :Wanajeshi wa kisomali walichangia sana katika kushinda kwa Imām. Shihab ad-Din, muislamu aliyekolea wa wakati ule ambaye aliandika kati ya miaka 1540 na 1560, na kuwataja sana mara kwa mara, (Futūḥ al-Ḥabasha, ed. na trs. R. Besset Paris, 1897.). Moja kati ya makundi maarufu ya kampeni hiyo walikuwa ni, Samaroon(Dir),Geri, Marrehān, na Harti---all Dārod na koo zao. Shihāb d-Dīn yuko wazi katika ugawaji wake wa maeneo kwa ajili ya mifugo, lakini nawaelezea waharti katika kipindi ambacho wao walikuwa wakiliki bandari ya Mait kwa upande wa Mashariki. Kwa upande wa Isaq, ni ukoo wa Habar Magadle ndio waliojumuishwa katika agawaji huu laki kumbukumbu zao hazikuoneshwa.Na hatimaye ukoo wa Dir ulichukua sehemu hiyo.

Matokeo ya utafiti huu, yanaongezewa nguvu katika kitabu cha hivi karibuni cha Oxford History of Islam:

TMtawala wa Adal, aliyeibuka na kuwa mmoja kati ya waislamu wenye misimamoi, inasemekana alikuwa akichukua wapiganaji wake kutoka katika jamii ya Wasomali.[1]

Lewis, kwa upande mwingine anagundua kuwa, asili ya Imam bado haijajulikana.Kuna ushahidi mwingine unoonesha kuwa, kuna uwezekano Mtawala huyu akawa Afar kwa asili. Eward anaunganisha jina la ʿAdäl na kabila la Dankali (Afar)Aḏaʿila na Jina la Kisomali kutoka katika ukoo wa Oda ʿAlï. Na kupendekeza kuwa, kuna uwezekano kuwa, Ufalme huu unawezekana kuwa ulijumuisha watu wa kabila Afars.[2] Japokuwa sehemu ya Afars inajumuisha sehemu kubwa ya of Adal, Didier Morin anasema kuwa, "Mwamko mkubwa wa ʿAfar upo juu ya ufalme wa `Adal bado ni wa wasiwasi kutokana na kuwa na makabila mbalimbali"[2] Nevertheless, Franz-Christoph Muth identifies Ahmad ibn Ibrihim al-Ghazi as Somali.[3]

Eneo la Ethiopia[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 1288, Adal lilikuwa ni eneo la Waislamu. Eneo la mtawala wa Kikristo wa Ethiopia aliyeitwaSolomonic Muda mfupi, baadae eneo hili lilipiganiwa na na kuwa chini na Ethiopia. negusä nägäst Amda Seyonna kampeni zake za mwaka 1332. Katika kipindi hiki, Mfalme wa Shewa Na Mfalme wa Ifat waliokuwa wakiongoza misafara ya kibiashara na bandari katika mwambao wa , pamoja na mfalme wa Zeila pia walitekwa.Baadae Adal ilikuja kuongozwa na Ifat, lakini baadea ilikuja kuwa huru baada ya mapigano yake dhidi ya Amde Seyon, lakini baadae tena, walijisalimisha baada ya Mfalme wao kufariki na kutekwa kwa mji mkuu wao wao Talag Na huo ndio ukawa mwisho Jamal ad-Din wa Ifat na ufalme wake. [4]

Katika mwaka kati ya 1403 au 1415, Waethiopia walivamia tena Ifat ambayo ndio tu ilikua imetoka katika mapigano, na kuweza kuwapiga maadui zao chini ya Mfalme wao. Sa'ad ad-Din II. Sa'ad ad-Din alifukuzwa kutoka katika utawala wao na ufalme wa Ethiopia, hii ikiwa ni mwaka 1403 au Yeshaq I in 1415) na baadae kuvamia eneo la Zeila na kumuua. Matokeo yake Familia za matajiri waliondoka nchini humona kukimbilia nchini Yemen kuepuka kukamatwa na kuuwawa. Walipokuja kurejea, walikuta tayari ufalme umebadilishwa kutoka jina la Mfalme wa Ifat na kuwa Mfalme Adal hii ikionesha kuwa, Ifat ilikuwa sehemu ya Adal.

Kuvamiwa kwa Ethiopia[hariri | hariri chanzo]

Katika miaka ya katika ya 1520 Imam Ahmad ibn Ibrihim al-Ghazi Aliivamia Adal na kutangaza rasmi vita takatifu dhidi ya wakristu wa Ethiopia.ambao kwa wakati huo walikuwa chini ta utawala wa Lebna Dengel. Wakiwa wanapewa zana za kupigania kutoka katika Ufalme wa Ottoman,. Ahmad aliweza kuwapiga waethiopia katika vita vya Battle of Shimbra Kure mwaka 1529, na kuweza kuchukua mali zote kutoka Ethiopia, kama vile maeneo ya mwinuko, japokuwa waethiopia waliendelea kukataa kuachia maeneo hayo. Mwaka 1541, Ureno ambayo ilikuwa wakihitaji baadhi ya maeneo katika Bahari ya Hindi, walituma msaada wa askari kwa Waethiopia. Na kwa kujibu suala hilo, Adal nao wakapokea askari 900 kutoka katika ufalme wa Ottomans

Imam Ahmad aliweza kufanikiwa katika mapigano dhidi ya Waethiopians, wakati akiendelea na kampeni katika Autumn mwaka 1542. Aliweza kumuua kiongozi wa kijeshi wa Ureno, Cristóvão da Gama mwezi Agosti mwaka huo huo. Hatahivyo wapiganaji wa Kireno walikataa kujisalimisha kutokana na kifo cha Adal katika vita vya Battle of Wayna Daga, karibu na ziwa Tana mwezi Februari mwaka 1543, ambapo Ahmad aliuwawa katika vita hivyo. Kutokana na hali hiyo, Waethiopia waliweza kuchuakua uwanda wa juu ulioinuka walioupateza baada ya kushindwa katika vita dhidi ya Adal. Mwaka 1577, mji mkuu wa Adal na uliamishiwa kutoka Zeila na kwenda Harar n hii ilifuatia kuanguka kwa utawala wa Adal.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mhariri John L. Esposito, The Oxford History of Islam, (Oxford University Press: 2000), p. 501
  2. 2.0 2.1 Herausgegeben von Uhlig, Siegbert, Encyclopaedia Aethiopica. Wiesbaden:Harrassowitz Verlag, 2003, pp.71
  3. ibid, pp. 155
  4. ibid, pp.71

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usultani wa Adal kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.