Nenda kwa yaliyomo

Negus Negesti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Negus Negesti ilikuwa cheo cha mfalme mkuu au Kaisari wa Ethiopia. Maana yake ni "mfalme wa wafalme".

Negus ni cheo cha kifalme kilichopatikana kwa watawala muhimu wa majimbo ya Ethiopia wenye kiwango kikubwa cha kujitawala chini ya mamlaka ya Negus Negesti.

Cheo hiki cha "Mfalme wa wafalme" kilianza kutumiwa na watawala wa Axum iliyokuwa dola kubwa la kwanza katika Ethiopia.

Negus Negesti wa mwisho alikuwa Haile Selassie kati ya 1930 hadi 1974 alipopinduliwa katika mapinduzi yaliyomaliza utawala wa kifalme katika Ethiopia.