Somaliland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Somaliland

Somaliland (kwa Kisomalia: Somaliland) ni eneo la kujitawala kaskazini mwa Somalia.

Hali halisi ni nchi huru tangu mwaka 1991 lakini haijatambuliwa na umma wa kimataifa, wala nchi nyingine yoyote.

Eneo lake ni karibu sawa na koloni la zamani la Somalia ya Kiingereza: jumla kilomita za mraba 137,600 iliyokuwa nchi huru kwa siku chache mwaka 1960 kabla ya kuungana na Somalia ya Kiitalia. Lakini kanda la mashariki linaloitwa Sanaag limejiunga na jimbo la Puntland ingawa linadaiwa na Somaliland kwa sababu ilikuwa sehemu ya koloni ya Kiingereza (angalia ramani ndogo upande wa kulia: Sanaag kwa rangi kijani-neupe).

Imepakana na Ethiopia, Jibuti, Ghuba ya Aden na jimbo la Puntland la Somalia.

Mji mkuu wa Somaliland ni Hargeisa.

Mikoa ya Somaliland
Somali lahoh (canjeero).
Maporomoko ya maji ya Lamadaya kwenye mlima Cal Madow.
Eneo la Somaliland.
Mandhari ya milima ya Cal Madow, makao ya spishi nyingi za pekee.
Ufukwe wa Berbera.
Dahabshiil huko Hargeisa.
Duka kubwa huko Burao.
Hargeisa International Airport huko Hargeisa.
Watu mjini Hargeisa.

Historia

Habari za kwanza zinazojulikana kuhusu eneo la Somaliland zasema lilikuwa chini ya milki ya Axum na baadaye Usultani wa Adal.

Bandari ya Berbera ilijulikana tangu zamani za Periplus ya Bahari ya Eritrea.

Katika karne ya 16 Waosmani waliingia wakishika utawala juu ya sehemu za magharibi kwa sababu walitaka kusimamia mlango wa Bahari ya Shamu, Bab el Mandeb.

Walifuatwa na Misri na baadaye Uingereza ambao uliitawala kama "British Somaliland Protectorate" au eneo lindwa la Somalia ya Kiingereza.

Koloni likapewa uhuru wake tarehe 26 Juni 1960 kama Nchi ya Somaliland, ikaungana baada ya siku tano na Somalia ya Kiitalia kuwa Jamhuri ya Somalia.

Wakati wa udikteta wa Siad Barre watu wa kabila la Isaaq waliteswa sana, wakaanza kuchukua silaha dhidi ya rais huyu.

Baada ya kuporomoka kwa serikali yoyote nchini Somalia, wazee wa eneo lililokuwa Somaliland walikutana na kuamua kurudisha uhuru wa awali.

Wakazi

Kuna wakazi milioni 4.5. Zaidi ya nusu ni wafugaji wa kuhamahama na takriban 45 % hukaa mjini au vijijini.

Karibu wote ni Wasomalia, hasa wa kabila la Isaaq, wengine ni wa Dir au Darood.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Somaliland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.