Berbera

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mahali pa Berbera

Berbera ni bandari na mji wa Somalia ya Kaskazini mwenye wakazi 260,000. Iko katika sehemu ya Somalia iliyojitenga kwa jina la Somaliland.

Mawasiliano na bandari[hariri | hariri chanzo]

Kuna kiwanja cha ndege na barabara za kuunganisha mji na Hargeysa na Burao.

Biashara ya bandari ilikuwa hasa kondoo, uvumba na mazao mengine ya Somaliland. Ethiopia imeanza kutumia bandari kwa biashara yake ya nje baada ya kutokea kwa mafarakano kati ya Ethiopia na Eritrea. Biashara ya Ethiopia inaleta mapata makubwa zaidi kwa bandari.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Bandari ya Berbera ni bandari bora upande wa kusini wa Ghuba ya Aden. Hali ya hewa ni joto sana na halijoto inaweza kupita sentigredi 50. Mazingira yake ni jangwa au nusujangwa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Habari za kwanza za mji ni Periplus ya Bahari ya Eritrea kitabu kilichoandikwa mnamo 200 BK. Wakati ule mji uliitwa "Malao". Historia yake ilifuata historia ya pwani kwa jumla; mara watawala wa kienyeji walikuwa na madola yao madogo, mara majirani makubwa yaliingia.

Tangu 1546 Dola la Osmani lilivamia eneo lote na kumpeleka wali wake Berbera. Wakati wa udhaifu wa Waturuki athira hii ilipotea tena. Baada ya vita ya Mahdi katika Sudani Waosmani walipaswa kuondoa wanajeshi wao tena na Waingereza waliingia wakaitawala Berbera kama sehemu ya eneo lindwa la "British Somaliland Protectorate" au Somalia ya Kiingereza.

Berbera ilikuwa bandari kuu ya Waingereza na pia makao makuu ya serikali yao wakati wa miezi isiyo na joto mno.

Baada ya uhuru wa Somali bandari ya Berbera ilikuwa na umuhimu fulani katika vita baridi kati ya Marekani ya Umoja wa Kisovyeti. Serikali ya Siad Barre 1974 ilifanya mapatano ya ushirikiano na Umoja wa Kisovyeti na manowari wa Kisovyeti zilipewa nafasi katika Berbera ikawa kituo cha kijeshi cha Kisovyeti. Ushirikiano huu ulifarakana tangu 1977 kwa sababu ya vita kati ya Somalia na Ethiopia na Wasovyeti walichagua kusimama upande wa Ethiopia. Barre alitafuta msaada wa Marekani na tangu 1981 Berbera ikawa kituo cha kijeshi cha Marekani.

Flag-map of Somalia.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Somalia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Berbera kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.