Hargeisa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru



Jiji la Hargeisa

Bendera

Nembo
Mahali paJiji la Hargeisa
Mahali paJiji la Hargeisa
Jiji la Hargeisa is located in Somaliland
Jiji la Hargeisa
Jiji la Hargeisa

Mahali pa mji wa Hargeisa katika Somaliland

Majiranukta: 9°33′47″N 44°4′3″E / 9.56306°N 44.06750°E / 9.56306; 44.06750
Nchi Somaliland
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 760,000

Hargeisa (kwa Kisomalia: Hargeysa; kwa Kiarabu: هرجيسا) ni mji mkuu wa Somaliland iliyojitenga na Somalia mwaka 1991. Iliwahi kuwa mji mkuu wa Somalia ya Kiingereza kuanzia 1941 hadi 1960. Kati ya 1960 hadi 1991 ilikuwa mji mkubwa wa pili wa Somalia.

Mji uko katika bonde kwenye kimo cha mita 1260 juu ya UB. Kimo kinasababisha hali ya hewa ya kupoa yaani hakuna joto kali jinsi ilivyo kwenye pwani ya Somaliland upande wa Ghuba ya Aden. Umbali na bandari ya Berbera ni km 160 kwa barabara.

Idadi ya wakazi hukadiriwa kuwa 760,000 (2015).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hargeisa kilikuwa ni kituo cha kijeshi cha Waosmani na Wamisri walipotawala Somalia ya Kaskazini. Tangu 1884 Waingereza walichukua nafasi ya Misri. Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia 1940 Italia ilivamia Hargeisa pamoja na Somalia ya Kiingereza kutoka Ethiopia. Baada ya kuwafukuza Waitalia mnamo mwaka 1941 Waingereza walihamisha mji mkuu wa koloni kutoka Berbera kwenda Hargeisa. Mnamo mwaka 1960 Hargeisa ilikuwa mji wa Somalia mpya baada ya maungano ya Somaliland na Somalia katika Kusini.

Katika miaka ya mwisho wa serikali ya dikteta Siad Barre Hargeisa ilikuwa kitovu cha upinzani wa watu wa kaskazini dhidi ya serikali ya Mogadishu. Mwaka 1988 mji uliharibiwa na mabomo ya jeshi la anga la Barre na watu 50,000 waliuawa. Somalia ilipoporomoka baada ya kifo cha Barre kuanzia mwaka 1990 eneo la Somaliland ikajitenga na Somalia. Hargeisa imeona kipidi kirefu cha utulivu na usalama ikaendelea kukua na kustawi.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Somaliland bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hargeisa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.