Puntland
Puntland (kwa Kisomali: Dowladda Puntland ee Soomaaliya, Dola la Puntland katika Somalia) ni jimbo la kujitegema la Somalia. Jimbo hili liko kwenye Somalia kaskazini-mashariki liko kamili kwenye ncha ya Pembe la Afrika.
Jina linatokana na nchi ya Punt ya Kale inayotajwa katika maandiko ya Misri ya Kale. Hadi leo haijulikani jina hili linataja kweli sehemu gani, lakini wataalamu wengi huamini ilikuwa mahali fulani kwenye pwani ya Somalia.[1]
Baada ya kuporomoka kwa Somalia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kuanzia mwaka 1991 viongozi wa eneo hili walijitangaza kuwa jimbo la kujitawala.[2] Tofauti na jirani yake Somaliland iliyotangaza uhuru wake, Puntland ilijipa katiba kama jimbo ndani ya Somalia ingawa hali halisi inajitawala tu.
Kwa jumla Puntand ilifaulu kutunza amani na kuepuka kushirikishwa katika vita ndani ya Somalia upande wa kusini.
Sehemu ya magharibi inayoitwa Sanaag inadaiwa pia na Somaliland kwa sababu sehemu hii iliwahi kuwa ndani ya Somalia ya Kiingereza wakati wa ukoloni, lakini wakazi waliamua kujiunga na Puntland.
Mji mkuu ni Garoowe lakini kitovu cha uchumi ni Boosaaso.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Idadi ya wakazi ni 4,284,633 kufuatana na kadirio la mwaka 2015. [3]
Lugha rasmi za serikali ni Kisomalia, Kiarabu na Kiingereza.
Wakazi wote ni Waislamu Wasunni. Uislamu ulitangazwa katika katiba kuwa dini rasmi na dini pekee linalokubaliwa. [4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Queen Hatasu, and Her Expedition to the Land of Punt Archived 6 Mei 2023 at the Wayback Machine., mlango 8 katika Pharaohs Fellahs and Explorers. by Amelia Edwards. New York: Harper & Brothers, 1891. (First edition.) pp. 261-300. Ilitazamiwa tar. 10 Januari 2017 kwenye tovuti ya http://digital.library.upenn.edu
- ↑ "Puntland State of Somalia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-21. Iliwekwa mnamo 2017-01-11.
- ↑ "Puntland Issues Report of population Estimation of Its Residents". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-04-30. Iliwekwa mnamo 2017-01-11.
- ↑ [web.archive.org/web/20071110124027/http://www.puntlandgovt.com/PuntlandConstitution.doc Archived 10 Novemba 2007 at the Wayback Machine. Katiba la Puntland, fungu 6]