Pembe la Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mataifa kwenye pembe la Afrika

Pembe la Afrika ni jina kwa sehemu ya mashariki kabisa ya bara la Afrika yenye umbo la pembetatu; ni kama rasi iliyoko kati ya Ghuba ya Aden na Bahari Hindi yenyewe.

Eneo hili linajumuisha nchi za leo za Somalia na Jibuti pamoja na sehemu ya mashariki ya Ethiopia; wakati mwingine Ethiopia yote pamoja na Eritrea huhesabiwa humo.

Nchani ya pembe iko Puntland iliyotangaza uhuru wake lakini inahesabiwa kama sehemu ya Somalia na mataifa mengi, jirani yake ni Somaliland ambayo ni pia sehemu ya Somalia iliyotangaza uhuru wake.

Kwa kutumia wazo la pembe la Afrika kubwa kuna eneo la 2,000,000 km² linalokaliwa na wakazi milioni 94.2 million (Ethiopia: milioni 79, Somalia: milioni 10, Eritrea: milioni 4.5 na Jibuti: milioni 0.7).