Somalia ya Kiitalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Somalia ya Kiitalia ndani ya Somalia ya leo

Somalia ya Kiitalia ilikuwa koloni ya Italia kwenye eneo la Somalia tangu miaka ya 1880 hadi 1960 mwaka wa uhuru.

Kuanzia 1888 Italia ilijipatia mikataba ya ulinzi na masultani mbalimbali waliotawala maeneo madogo kwenye pembe la Afrika. Walitangulia 1889 na sultani ya bandari ya Hobyo na mtawala wa usultani wa Majerteen.

Mwaka 1892 Usultani wa Zanzibar alikodi mabandari ya Banadir kati ya Mogadishu hadi Brava kwa Italia. 1905 Italia ilinunua eneo hili kutoka Zanzibar na kulitangaza kuwa koloni na Mogadishu kuwa mji mkuu.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Waitalia walikabidhiwa eneo la Kismayu kutoka Uingereza. Walilitawala kwa jina la "Oltre Giuba" (ng'ambo ya mto Juba) na kuliunganisha na Somalia ya Kiitalia tar. 30 Juni 1926.

Wakati uleule waliamua kumaliza hali ya sultani za Majarteen na Hobyo kuwa nchi lindwa na kuzifanya sehemu kamili za koloni. Mipango hii ilisababisha vita kali ya miaka miwili kwa sababu masultani waliona mikataba yao ya ulinzi ilivunjwa wakapinga jeshi la Italia.

Mwaka 1936 Somalia ikaunganishwa na Ethiopia kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kiitalia.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia koloni ya Italia ilivamiwa na Uingereza tangu 1941. 1949 Somalia ilirudishwa mkononi mwa Italia kwa niaba ya Umoja wa Mataifa.

Mwaka 1960 utawala wa kikoloni ulikwisha na Somalia ikapata uhuru wake.