Ukhalifa wa Cordoba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ukhalifa wa Cordoba (Ar.خلافة قرطبة‎; Khilāfat Qurṭuba) ilikuwa milki kubwa kilichounganisha Al-Andalus iliyokuwa sehemu ya kiislamu ya Rasi ya Iberia (Ureno na Hispania ya leo) kati ya 929 na 1031. Mji mkuu alikotawala khalifa ilikuwa Cordoba.

Emirati ya Cordoba[hariri | hariri chanzo]

Historia ya milki hii ilianza mwaka 756. Mwaka ule Abd-ar-Rahman I alikuwa emir wa eeneo la Cordoba katika Al-Andalus (Hispania) mnamo 756. Alizaliwa katika nasaba ya Wamuawiya huko Shamu akakimbia kutoka nchi yake baada ya kupinduliwa kwa nasaba hii mwaka 750. Emirati ya Cordoba iliendelea kati ya madola ya Al-Andalus na kupata nafasi ya kwanza.

Ukhalifa[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 929 amiri Abd-ar-Rahman III aliamua kutumia cheo cha khalifa. Chini ya utawala wake na wafuasi wake Codoba ilikuwa kitovu cha utamaduni kuu katika Ulaya.

Makhalifa wa mmwisho hawakutawala tena wenyewe walitegemea washauri na wakubwa wao. Mwaka 1031 ukhalifa uliporomoka ukagawiwa kwa madola madogo.