Orodha ya nasaba za Kichina

Maeneo yaliyotawaliwa na nasaba mbalimbali katika urefu wote wa historia ya China.
Orodha hii inataja nasaba za kifalme za Kichina na vipindi vinginevyo katika historia ya Uchina.
- Nasaba ya Xia (2070 KK- 1600 KK)
- Nasaba ya Shang (karne ya 16 KK hadi 1046 KK)
- Nasaba ya Chou (1046 KK hadi 256 KK)
- Nasaba ya Ch'in (221 KK hadi 207 KK)
- Nasaba ya Han (202 KK hadi mwaka wa 220)
- Wakati wa San-Guo au "Nchi Tatu" (kuanzia 220 hadi 280)
- Nasaba ya Hsi Chin (kuanzia 266 hadi 316)
- Nasaba ya Dong Jin (kuanzia 317 hadi 420)
- Uvamizi wa Hsiung-nu (kuanzia 304 hadi 439)
- Nasaba ya Wei (kuanzia 386 hadi 534)
- Nasaba ya Sui (kuanzia 581 hadi 618)
- Nasaba ya Tang (kuanzia 618 hadi 907)
- Wakati wa Shih-Kuo au "Nchi Kumi" (kuanzia 907 hadi 960)
- Nasaba ya Sung (kuanzia 960 hadi 1279)
- Nasaba ya Yüan (kuanzia 1215 hadi 1368)
- Nasaba ya Ming (kuanzia 1368 hadi 1644)
- Nasaba ya Ch'ing (kuanzia 1636 hadi 1912)
Baada ya hapo hakuna nasaba ya kifalme tena, kwa sababu China imekuwa jamhuri.