Jamhuri ya Watu wa China

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Zhonguo.jpg
Zhōnghuá Rénmín Gònghéguó

Jamhuri ya Watu wa China
Bendera ya China Nembo ya China
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Maandamano ya wale wanaojitolea - ''Yìyǒngjūn Jìnxíngqǔ''
Lokeshen ya China
Mji mkuu Beijing
km²) 39°55′ N 116°23′ E
Mji mkubwa nchini Shanghai
Lugha rasmi Mandarin Kichina1 (Putonghua)
Serikali Ujamaa republic2
Xi Jinping
Wen Jiabao
Tarehe za kihistoria
Utawala wa nasaba ya Shang
Utawala wa nasaba ya Qin
Jamhuri ya China
Jamhuri ya Watu wa China ilitangazwa

1766 KK
221 KK
10 Oktoba 1911
1 Oktoba 1949
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
9,596,960 km² km² (ya 33)
2.82
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
1,315,844,0004 (ya 1)
1,242,612,226
140/km² (ya 72 (2))
Fedha Renminbi Yuan5, 2 (CNY)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+8)
not observed (UTC+8)
Intaneti TLD .cn2
Kodi ya simu +862

-

1 Pamoja na Kichina cha Mandarin kile cha Kikanton ni lugha rasmi katika Hong Kong na Macau. Kiingereza ni pia lugha rasmi katika Hong Kong na Kireno huko Macau. Vilevile kuna lugha za kieneo yanayotumiwa rasmi kama vile Kiuyghur huko Xinjiang, Kimongolia katika jimbo la Mongolia ya Ndani, Kitibet huko Tibet na Kikorea katika mkoa wa Yanbian.


China (pia: Uchina, Sina) au Jamhuri ya Watu wa China, ni nchi kubwa ya Asia ya Mashariki na nchi yenye watu wengi duniani.

China imepakana na Vietnam, Laos, Myanmar, India, Bhutan, Nepal, Pakistan, Afghanistan, Tajikistan, Kyrgyzstan, Kazakhstan, Urusi, Mongolia, Korea ya Kaskazini. Kuna pwani ndefu la Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China ambazo ni bahari ya kando ya Pasifiki. Mji mkuu ni Beijing.

China kuna makabila tofauti 56. Walio wengi (92%) ni Wahan. Lugha rasmi ni Kichina cha Mandarin. Siasa inatawaliwa na chama cha kikomunisti.

Mji mkuu ni Beijing na Shanghai ni mji mkubwa. Hong Kong iliyokuwa koloni ya Uingereza na Macau iliyokuwa koloni ya Ureno ni maeneo ya China yenye utawala wa pekee.

Taiwan na visiwa vingine vya Jamhuri ya China vinatazamiwa na serikali ya Beijing kuwa majimbo chini yake lakini vimekuwa kama nchi ya pekee tangu 1949.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

China ina eneo la kilomita za mraba 9.6 hivyo ni nchi kubwa ya tatu au ya nne [1] duniani.

Sura ya nchi yake inaonyesha tabia tofautitofauti. Upande wa kaskazini mpakani na Siberia na Mongolia kuna maeneo yabisi pamoja na jangwa la Gobi. Kinyume chake upande wa kusini mpakani wa Vietnam, Laos na Burma hali ya hewa ni nusutropiki yenye mvua nyingi unaolisha misitu minene. Sehemu za magharibi zina milima mingi ambayo ni kati ya milima mirefu duniani kama Himalaya na Tian Shan. Mashariki ya nchi huwa na tambarare zenye rutba na hapa ndipo kanda lenye wakazi wengi. Pwani za bahari zinapakana na Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China.

Upana wa China kati ya kaskazini na kusini ni kilomita 4,200 na kati ya mashariki na magharibi ni kilomita 4,200. Pwani lina urefu wa kilomita 14,400.

Kuna mito mikubwa; mrefu zaidi ni Yangtse (6,300 km), Hwangho au Mto Njano, Xi Jiang au mto wa Magharibi, Mekong, Mto wa Lulu, Brahmaputra na Amur. Mito hii yote ina vyanzo vyao katika milima mikubwa penye usimbishaji mwingi ikibeba maji kwenda tambarare pasipo na mvua nyingi. Jiografia hii ilikuwa chanzo cha kilimo cha umwagiliaji na kukua kwa madola ya kwanza.

Kutokana na madawa ya kilimo na maji machafu ya viwanda mito na maziwa ya China hupambana na machafuko makali; mwaka 2007 ziwa Tai lilisafishwa kwa gharama kubwa mno kwa sababu maji hayakufaa tena kwa mahitaji ya maji ya bomba.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Kanda za usimbishaji za China

Kuna kanda 18 za hali ya hewa zonazoonyesha tofauti kubwa kati yao. Upande wa magharibi, kaskazini na kaskazini-mashariki huwa na majira yenye joto kali na baridi kali. Upande wa kusini ina tabia ya tropiki au nusutropiki. Tibet huwa na hali ya hewa kulingana na kimo chake juu ya mita 4,000.

Ramani ya usimbishaji inaonyesha ya kwamba kilimo kinawezekana katika nusu ya kusini na kusini-mashariki ya nchi tu. Upande wa kaskazini na magharibi mvua ni mkidogo mno. Mstari mwekundu unaonyesha mpaka na juu yake usimbishaji ni chini milimita 390 kwa mwaka.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

China ina wakazi milioni 1,300 ni nchi yenye watu wengi duniani. Historia yake yote iliona tena na tena vipindi vya njaa kutokana na idadi kubwa ya watu wake. Msongamano wa watu kwa wastani ni wakazi 135 kwenye kila kilomita ya mraba. Lakini tofauti ziko kubwa kati ya miji mikubwa ambako milioni 115 wanakaa kwenye eneo la 50,000 km² na Tibet penye watu 2 tu kwa kilomita ya mraba.

Wakazi walio wengi ni Wahan au Wachina wenyewe. Wanatumia lahaja za lugha ya Kichina. Pamoja na Wahan kuna makabila 55 yaliyotambuliwa na serikali.

Zaidi ya asilimia 90 za wakazi wote wanakaa katika theluthi ya kusini-mashariki ya nchi penye mvua ya kutosha. Ndani ya theluthi hili ni nusu ya Wachina wote wanaosongamana kwenye asilimia 10 za China yote maana yake katika 10% hizi kuna msongamano wa watu 740 kwa km².

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya China huganwanyika katika vipindi vya nasaba za kifalme mbalimbali. Vipindi muhimu zaidi ni kama zifuatazo:

Utawala wa kifalme uliendelea hadi mapinduzi ya Kichina ya 1911.

Baada ya kipindi cha mvurugo jamhuri ya China ilitawaliwa na chama cha Kuomintang chini ya rais Chiang Kai-shek. Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia sehemu kubwa ilitwaliwa na Japani. Katika wakati huu Chama cha Kikomunisti cha China kilijenga jeshi kikapambana na serikali ya Kuomintang na Japani pia. Baada ya mwisho wa vita kuu Wakomunisti waliendelea kupingana na serikali na 1949 Kuomintang ilishindwa. Wakomunisti chi ya Mao Zedong walianza kutawala China Bara kama Jamhuri ya Watu wa China na Kuomintang walikimbia kisiwa cha Taiwan walipoendelea kutawala kama "Jamhuri ya China".

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Serikali ya China inatawala kwenye mfumo wa udikteta chini ya uongozi wa Chama cha Kikomunisti ya China. Kuna vyama vidogo lakini hivi havina umuhimu wowote vinasimamiwa na Wakomunisti halisi halisi ni mfumo wa chama kimoja.

Kikatiba chombo kikuu ni Bunge la umma la China linalomchagua rais, serikali, mahakama kuu, kamati kuu ya kijeshi na mwanasheria mkuu. Lakini hali halisi maazimio yote ya bunge ni utekelezaji tu wa aazimio ya uongozi wa chama cha kikomunisti.

Uongozi huu ni kundi dogo la wakubwa wa chama na jeshi. Mwanasiasa muhimu ni mwenyekiti Hu Jintao. Kwa sasa yeye anaunganisha vyeo vya Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi. Alichaguliwa mwaka 2002 kuwa Katibu Mkuu cha chama lakini hakuwa mwenyekiti wa kamati ya kijeshi hadi 2004. Kwa jumla katika mapokeo ya kikoministi vyeo vya chama ni muhimu kuliko vyeo vya serikali ingawa katiba na sheria inasema tofauti.

Kuna pia "maeneo yenye utawala wa pekee" ambayo ni Hongkong na Macao. Katika miji hii miwili iliyokuwa kolini za Uingereza na Ureno kuna uhuru wa kisiasa na wa majarida, uchaguzi huru na upinzani kamili lakini maeneo yana tu madaraka kadhaa ya kujitawala kwa mambo ya ndani.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Baada ya Urusi na Kanada ambazo ni nchi mbili kubwa China na Marekani ni karibu sawa; kama maeneo yanayodaiwa na China bila kukubaliwa na majirani yanahesabiwa mle baso China ni kidogo kubwa kuliko Marekani
Flag-map of the People's Republic of China.svg Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Watu wa China kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.