Nenda kwa yaliyomo

Nyanda za juu za Tibet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyanda za juu za Tibet ziko kati ya safu za Himalaya upande wa kusini na safu ya Kunlun kwenye kaskazini.
Himalaya jinsi inavyoonekana kutoka satelaiti katika anga-nje, kutazama upande wa kusini.

Nyanda za juu za Tibet ni eneo kubwa la milima na tambarare ambayo ni angalau mita 4,000 au zaidi juu ya usawa wa bahari katika Asia ya Kati. Zinaenea katika Mkoa wa Tibet wa China, Mkoa wa Qinghai nchini China, na Ladakh huko Kashmir, Uhindi. Sehemu kubwa kabisa iko chini ya mamlaka ya China.

Nyanda hizo za juu huwa na eneo la kilomita za mraba milioni 2 hivi. Nchi hiyo pana inayolingana kwa ukubwa wa Tanzania mara mbili inakaliwa na watu wasiozidi milioni 10 pekee. Sababu ni baridi kali katika sehemu nyingi za milima hiyo na pia uhaba wa mvua; usimbishaji wa mwaka ni kati ya milimita 100 hadi 300 kwa mwaka ukinyesha zaidi kama mvua ya mawe (barafu). Katika seheu ambako baridi haizidi kuna uoto wa nyasi unaoruhusu maisha ya wafugaji wa kuhamahama.

Hata hivyo mito mikubwa ya Asia kama vile Mekong, Mto Njano, Mto Yangtze, Brahmaputra na Indus ina vyanzo vyake kwenye theluji na barafu ya barafuto za nyanda za juu za Tibet.

Nyanda za juu za Tibet ziliundwa na nguvu zilezile zilizokunja milima ya Himalaya na kuiinulia, yaani nguvu ya mwendo wa bamba la Uhindi unaosukuma dhidi ya bamba la gandunia chini ya Asia.

Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za juu za Tibet kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.