Tibet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Tibet-claims.jpg
            Tibet ya kihistoria jinsi inavyodaiwa na harakati za uhuru kwa nchi
Maeneo ya Watibet jinsi yanavyotajwa na Jamhuri ya Watu wa China
Eneo la Mkoa wa kujitawala wa Tibet ndani ya China (hali halisi)
Eneo linalodaiwa na Uhindi
Eneo linalidaiwa na China kama sehemu ya Mkoa wa kujitawala wa Tibet
Maeneo mengine ambayo kihistoria yalikuwa chini ya athira ya Tibet
Ramani ya Tibet ya Kichina

Tibet ni nchi katika milima ya Himalaya ya Asia. Mji mkuu ni Lhasa. Watibet walio wengi ni Wabuddha.

Tibet imekuwa sehemu ya Jamhuri ya Watu wa China tangu miaka ya 1950.

1951 China ilishambulia jeshi la Tibet ikalazimisha serikali ya Tibet kukubali ya kwamba ni sehemu ya China; ikaahidiwa ya kwamba mamabo ya ndani yataendelea jinsi ilivyokuwa awali. Lakini mnamo 1958 maafisa wa China walianza kumtendea Dalai Lama (kiongozi wa Tibet) kwa udharau. Dalai Lama alikimbilia Uhindi na jeshi la China likakandamiza harakati ya watu ya kurudisha uhuru wa nchi.

Tangu 1959 kuna Watibet wengi wanaokaa Nepal na Uhindi kama wakimbizi. Ndani ya Tibet idadi ya walowezi Wachina iliongezeka.