Gandunia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Gandunia (kutoka maneno "ganda" na "dunia") ni mafundisho ya sayansi za jiolojia na jiofizikia kuhusu tabia za ganda la dunia na miendo ya sehemu zake.

Tectonic plates (surfaces are preserved)

Muundo wa dunia[hariri | hariri chanzo]

Inaanza na hoja la kuwa muundo wa dunia ni wa tabaka mbalimbali. Tabaka imara ni ganda la nje la dunia pamoja na sehemu ya juu ya koti ya dunia chini ya ganda hili. Tabaka hii -inayoitwa "tabakamwamba"- inakaa juu ya tabaka moto na laini.

Ndani ya tabaka hili laini kuna mwamba katika hali ya geli yaani ni kati ya hali imara na hali kiowevu. Kwa hiyo vipande vyake havikai mahali pamoja lakini vina mikondo ndani yake kufuatana na mikondo ya joto kali inayopanda juu kutoka kiini cha dunia ambacho ni chuma ya moto katika hali kiowevu.

Mikondo hii inasukuma dhidi ya tabakamwamba ya nje na kuivunjavunja katika vipande au mabamba mbalimbali.

Mikondo ya joto ndani ya dunia husababisha kutokea kwa miamba mipya kwenye migongo ya sakafu ya bahari na kuzama kwa kando la mabamba ya kibahari chini ya mabamba ya kibara

Mwendo wa mabamba[hariri | hariri chanzo]

Kufuatana na nadharia ya gandunia ganda la nje limevunjika na vipande vya ganda vyaitwa mabamba. Mabamba haya yakaa juu ya koti moto kama majani inayofunika maji katika sufuria inayopashwa moto. Maji ya moto huzunguka ndani ya sufuri na kusababisha majani usoni kutembea. Hivyo mabamba ya gandunia yana mwendo wakati wote. Mwendo huu husababishwa na kupaa juu kwa magma (yaani mwamba moto wa kiowevu) inayotoka nje kwenye migongo iliyoko katikati ya sakafu ya bahari. Migongo hii ni safu ya milima ya kivolkeno chini ya maji, kwa mfano mgongo kati wa Atlantiki.

Magma hii inapoa kuwa mwamba mpya na kusukuma nusu mbili za bamba la kibahari kwenda nje. Pale ambako bamba la kibahari inapokutana na bamba la bara linajisukuma chini yake kwa sababu miamba ya mabara ni nyepesi na miamba ya bamba la kibahari ni nzito zaidi. Hivyo pembizo la bamba la kibahari linazama chini na kuyeyuka katika joto la koti ya dunia. Eneo la kuzama chini linanonekana mara nyingi kama mfereji chini ya bahari.

Shindikizo hili la sakafu ya bahari linasababisha pia mwendo wa bamba la kibara pamoja na kuvunjika kwa mabamba ya kibara.

Gandunia na uso wa dunia[hariri | hariri chanzo]

Miendo ya gandunia imeunda uso wa dunia jinsi ilivyo na jinsi inavyoendelea kutokea na kubadilika.

  • kugongana kwa mabamba husababisha kukunja kwa ganda la dunia na kutokea kwa nyororo za milima.
  • kuzama kwa pembizo la bamba moja chini ya bamba lingine husababisha kutokea kwa mifereji chini ya bahari na volkeno kwenye bamba la juu - au kutokea kwa nyororo ya visiwa vya kivolkeno kwenye mstari wa kuzama. Maeneo haya kuna mitetemeko ya ardhi mara kwa mara.
  • shindikizo ya gandunia husababisha pia kuvunjika kwa mabamba. Hali hii inaonekana kwa kutokea kwa mabonde ya ufa.
WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Gandunia" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gandunia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.