Nenda kwa yaliyomo

Bamba la gandunia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mabamba gandunia ya dunia yetu.

Bamba gandunia ni jina lililobuniwa hivi karibuni[1] kwa mapande yanayounda sehemu ya nje ya dunia yetu. Sehemu hiyo ya nje huitwa ganda la dunia na chini yake kuna sehemu ya dunia ambayo ni ya joto kiasi ya kwamba miamba na elementi zote zinapatikana katika hali ya giligili yaani kuyeyushwa. Hiyo sehemu ya nje ya dunia si pande moja bali kuna mapande mbalimbali kandokando yanayoelea juu ya mata ya moto ndani yake. Unaweza kusoma zaidi katika makala kuhusu muundo wa dunia.

Gandunia ni elimu kuhusu ganda la dunia. Hoja ya sayansi kuhusu gandunia ni kwamba ganda la dunia limevunjika mapandemapande yanayoitwa mabamba. Kila bamba linapakana na mabamba mengine. Mabamba yasukumwa na mikondo ya moto chini yake kama majani yanayokaa usoni mwa maji yanayoanza kuchemka katika sufuria. Hivyo kila bamba lina mwendo wake wa pekee pamoja na au dhidi ya mabamba mengine. Tetemeko la ardhi ni dalili ya kwamba mabamba yamesuguana na hivyo kusababisha mishtuko tunayojua kama tetemeko la ardhi.

Mabamba hayo ni sehemu ya nje ya tabakamwamba (lithosferi). Tabaka hilo limevunjika katika mapande makubwa 7 na vingine vidogo vinavyoelea juu ya tabaka lenye hali ya kiowevu chenye mnato mzito.

Mabamba hayo yote yameonekana kuwa na mwendo wa sentimita kadhaa (cm 2 - 20 zimepimwa) kwa mwaka. Mwendo huo husababishwa na nguvu ya magma (mwamba moto wa kiowevu) inayopanda juu na kusukuma mabamba hayo.

Mabamba makuu ya dunia[hariri | hariri chanzo]

Mabamba makubwa ya ganda la nje ya dunia ni:

Kati ya mabamba madogo kuna:

Mwendo wa mabamba: jinsi Pangaea ilivyosambaratika na kutokea kwa mabara ya leo.

Mwendo wa mabamba[hariri | hariri chanzo]

Mwendo wa mabamba hayo umesababisha kutokea na kuvunjika kwa mabara katika historia ya dunia yetu.

Wataalamu hufikiri ya kwamba dunia ilikuwa na bara kubwa moja tu (Pangaea) miaka milioni 300 - 150 iliyopita iliyovunjika katika mapande au mabamba mbalimbali.

Hata mabamba yaliyopo kwa sasa yanatarajiwa kuendelea kuhamahama, kuvunjika au kupotea kabisa.

Kwa mfano Afrika iko katika mwenendo wa kupasuliwa kwenye mstari wa Bonde la Ufa yaani Afrika ya Mashariki inaelekea kujitenga na sehemu nyingine ya bara ikiwa bamba la pekee. Penye Bonde la Ufa la sasa bahari itatanda baada ya miaka milioni 20.

Bara Hindi au bamba la Uhindi inaendelea kugonga bamba la Asia na kujisukuma chini ya milima ya Himalaya - kuna uwezekano ya kwamba itaingia kabisa na kutoweka.

Makala hiyo kuhusu "Bamba la gandunia" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

  1. Neno gandunia si kawaida bado, tunafuata hapo kamusi ya KAST.