Sentimita

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Cm)
rula ya seremala katika mgawanyo wa sentimita

Sentimita (pia: sentimeta; kifupi: cm) ni kipimo cha urefu. Ni sawa na sehemu ya mia moja au asilimia moja ya urefu wa mita ambayo ni kipimo cha kimataifa cha SI.

Kipimo cha kulingana kwa eneo ni sentimita ya mraba (cm²).

Sentimita si kiwango rasmi katika utaratibu wa SI, lakini inafaa sana katika matumizi ya kila siku. Sentimita moja huwa ni upana wa kucha ya kidole cha mtu mzima.

millimita << sentimita << desimita << mita << kilomita

Ulinganisho na vipimo vingine[hariri | hariri chanzo]

Sentimita moja ni sawa na:

  • 0.01 mita
  • 0.3937 inchi (inchi 1 ni 2.54 sentimita)

Tazama[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]