Addis Ababa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jiji la Addis Ababa
Skyline ya Jiji la Addis Ababa
Jiji la Addis Ababa is located in Ethiopia
Jiji la Addis Ababa
Jiji la Addis Ababa
Mahali pa mji wa Addis Ababa katika Ethiopia
Anwani ya kijiografia: 9°1′48″N 38°44′24″E / 9.03°N 38.74°E / 9.03; 38.74
Nchi Ethiopia
Idadi ya wakazi
 - 2,738,248
Tovuti: www.addisababacity.gov.et
Ramani ya Ethiopia ikionyesha Addis Ababa
Addis Ababa, inavyo onekana kutoka anga.

Addis Ababa (pia Addis Abeba; kwa Kiamhara አዲስ አበባ, "Ua Jipya"; kwa Kioromo Finfinne) ni mji mkuu wa Ethiopia na wa Umoja wa Afrika.

Ina cheo cha mji wa kujitawala (ras gez astedader) kama jimbo la Ethiopia.

Mji wenyewe una watu kutoka makabila 80, wakiongea lugha 80, na jamii za Waislamu na Wakristo.

Addis Ababa iko mita 2,500 juu ya usawa wa bahari kwa 9.03° N 38.74° E). [1]

Eneo hii lilichaguliwa na Malkia Taytu Betul na Mji kuanzishwa mwaka wa 1886 na bwana yake, Mfalme Menelik II, na sasa mji huu una umma milioni nne, na asilimia nane ya ukuzi wa uchumi.

Mji huu uko kwa tako la Mlima Entoto, na ni makazi maalum ya Chuo Kikuu cha Addis Ababa. Chuo Kikuu cha Addis Ababa kilijulikana kama Chuo Kikuu cha Haile Selassie I, kutokana na jina la Mfalme wa mwisho wa Ethiopia, ambaye alitoa jumba ya mfalme (Jumba Guenete Leul) iwe makao maalum ya Chuo Kuu ya Addis ababa mwaka wa 1961.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Addis Ababa ilianzwa na Mfalme wa Ethiopia Menelik II. Menelik, kama mfalme wa Shewa, aligundua mlima Entoto kama kambi nzuri sana ya jeshi ili kumiliki upande wa kusini, na mwaka wa 1879 alitemembea kwa mibomoko ya kale ya mji huu, na kuona kanisa ambayo ujenzi haukuwa umemalizwa, kuthibati kua Waithiopia waliishi kwa mji huu kabla ya vita za Ahmad Gragn. Masilahi ya Menelik wa pili iliongezeka, Mke wake alipoanza kazi ya ujezi wa kanisa eneo Entoto, na Menelik kuamri kanisa la pili eneo hiyo. Lakini eneo hiyo haikutua kuwa mji haraka kwa sababu ya ukosefu wa kuni na maji, na makazi hasa ilianzia kwa bonde kusini mwa mlima mwaka wa 1886. Mwanzo, Taytu alijijengea nyumba karibu na "Filwoha" chemchem moto iliyo na madini, ambayo ya julikana na waenyeji Waoromo kama Finfinne, Malkia Taytu na watumishi Washowan wa kifalme walipenda sana kuoga kwa maji hayo ilionamadini. Washarifu wengine na Watumishi na mali yao, wao pia walikaa sehemu hii, na menelik kuongeza jumba la Mke wake, ili iwe Jumba Rasmi la Miliki ambayo ndio makazi rqasmi ya serikali Addis Ababa mbaka wa leo. Menelik wa pili kaanza Addis Ababa kama Mji Mkuu wa Ethiopia. Moja wapo ya maendeleo Menelik alifanya nikama, kupanda miti ya eucalyptus kwa mitaa kando ya barabara.

Mwaka wa 1936, Jeshi la Waitaliano lilitwaa Addis Ababa kwa Vita vya Pili vya Waitaliano na Wahebeshi, na kuifanya Addis Ababa Mji Mkuu Italia Ya Afrika Mashariki. Addis Ababa iliongozwa na govana Magavan Waitaliano wa Addis Ababa kutoka mwaka wa 1936 mpaka 1939. Baadaye Waitaliano kwa kupingwa na wazalendo wa Ethiopia, na pia kushidwa vita na Waithiopia kwa usaidizi wa Waiingereza kwa kampeni ya Afrika Mashariki na pia ukombozi wa Ethiopia, Mfalme Haile Selassie alirudi Addis Ababa mnamo Mai 5, 1941 -- Baada ya miaka mitano kamili, na kuanza kazi ya kuendeleza Mji Mkuu, Addis Ababa.

Mfalme Haile Selassie alisaidia kuanzisha Organization of African Unity mwaka 1963 akaikaribisha kuwa na makao makuu mjini. Ilipogeuka kuwa Umoja wa Afrika mwaka 2002, makao yakabaki yaleyale.

Zaidi ya asilimia 51% ni wanawake.
Addis Ababa Majengo Kutoka: whileseated.org

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: