Dini za jadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mganga wa kienyeji wa mwanzo wa karne ya 20 wa kabila la Waigbo huko Nigeria, Afrika Magharibi.

Dini za jadi ni dini za mababu ambazo zinafuata miiko na maadili halisi ya taifa au kabila fulani.

Katika bara la Afrika dini hizo zinaegemea zaidi kwenye matambiko kwa mizimu ya ukoo ili isaidie jamaa zao.

Siku hizi idadi ya wafuasi wa dini hizo inazidi kupungua na kuziachia nafasi dini za kimataifa, hasa Ukristo na Uislamu.

Hata hivyo mabaki ya imani ya asili yanawaandama waliojiunga na dini hizo, hasa kwa namna inayotazamwa nazo kuwa ushirikina.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Magesa, Laurenti. 1997. African Religion. The Moral Traditions of Abundant Life, Maryknoll: Orbis. ISBN 1-57075-105-6