Niger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kwa maana nyingine ya neno "Niger" tazama Niger (maana).

République du Niger
Jamhuri ya Niger
Bendera ya Niger Nembo ya Niger
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Fraternité, Travail, Progrès
(Undugu, Kazi, Maendeleo)
Wimbo wa taifa: La Nigerienne
Lokeshen ya Niger
Mji mkuu Niamey
13°32′ N 2°05′ E
Mji mkubwa nchini Niamey
Lugha rasmi Kifaransa
Serikali Jamhuri
Mahamadou Issoufou
Brigi Rafini
Uhuru
imetangazwa
kutoka Ufaransa
3 Agosti 1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,267,000 km² (ya 22)
0.02%
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2012 sensa
 - Msongamano wa watu
 
11,665,937 (ya 69)
17,138,707
12.1/km² (ya 175)
Fedha Franki ya CFA (XOF)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+1)
(UTC+2)
Intaneti TLD .ne
Kodi ya simu +227

-


Ramani ya Niger.

Niger (pia Nijeri) ni nchi kubwa zaidi ya Afrika ya Magharibi kwa eneo.

Imepakana na Algeria na Libya upande wa kaskazini, Mali na Burkina Faso upande wa magharibi, Chad upande wa mashariki na Nigeria pamoja na Benin upande wa kusini.

Mji mkuu ni Niamey, kusini mwa nchi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Niger haina pwani kwenye bahari yoyote.

Ni sehemu ya kanda la Sahel, yaani sehemu kubwa ya nchi ni yabisi, kaskazini mwake ni yabisi sana ikiwa jangwa la Sahara.

Ardhi yenye rutuba iko kusini kabisa, karibu na mto wa Niger.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Mipaka ilichorwa wakati wa ukoloni wa Ufaransa, ikiunganisha watu wenye utamaduni tofautitofauti, kama vile Watuareg (10.4% za wakazi wote) wa Sahara, wahamaji Wafula (9.9%) na Wakanuri (4.4%) wa eneo la Sahel na wakulima wa kusini kama Wasonghai (21.2%) na Wahausa: hawa wa mwisho ni 53% .

Tofauti hizo kubwa zilileta kipindi cha ugomvi kati ya makabila uliopoa tena baada ya mwaka 2000. Tatizo kubwa la nchi ni vipindi vya ukame na njaa vinavyorudiarudia mara kwa mara.

Wakazi walikuwa zaidi ya milioni 17 katika sensa ya mwaka 2012. Idadi kubwa wako kusini.

Kadiri ya utafiti wa mwaka 2005, asilimia 8 walikuwa watumwa.

Tangu wakati wa ukoloni, lugha rasmi ni Kifaransa. Lakini kuna lugha 8 za taifa kati ya lugha kuu za makabila asili. Muhimu zaidi ni Kihausa na Kizarma-Sonrai.

Walio wengi kabisa (99%) ni wafuasi wa Uislamu, waliokadiriwa kuwa 94-97% za wananchi wote; sehemu yao wanasemekana kuchanganya Uislamu na dini asilia za Kiafrika. Wakristo ni 0.4% tu. Hata hivyo Niger ni nchi isiyo na dini rasmi.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Niger kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.