Njaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mama na mtoto wenye njaa wakati wa maangamizi ya Waashuru chini ya Waturuki, 1915.

Njaa ni hali ya kukosa chakula kinachohitajiwa na mwili ili kujimudu.

Sababu zake zinaweza kuwa mbalimbali, kama vile vita, ukame, maradhi ya mimea, wadudu waharibifu, utovu wa ustadi katika uzalishaji na utunzaji wa mazao, ugumu wa mawasiliano n.k.

Kila bara liliwahi kupatwa na hali hiyo katika historia, na bado hiyo ni tishio kwa nchi mbalimbali, pia kutokana na sababu mpya, kama vile utandawazi, matumizi ya mazao kwa ajili ya kuendesha mashine kiekolojia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: