Nenda kwa yaliyomo

Utandawazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bango la biashara la McDonald's kwa Kiarabu. Utandawazi unaendana na makampuni mengi kuenea duniani kote.

Utandawazi (kwa Kiingereza globalization) ni neno lililoanza kutumika miaka ya 1990, likimaanisha kukifanya kitu kuwa katika kiwango cha kimataifa, na kukihamisha nje ya mipaka na kukifanya kuwa cha wazi na kikafanywa na watu wa aina zote duniani.

Utandawazi ni njia ambayo wenyeji au taifa hufanya mambo kuwa ya kimataifa, kufanya mambo pamoja duniani. Inahusu suala zima la uchumi au biashara, teknolojia, siasa na utamaduni vilevile.

Utandawazi pia una maana ya jambo linalolenga umiliki wa kifikra na wa kiutamaduni juu ya tamaduni nyingine zilizo dhaifu, kwa ajili ya kusaidiana na kuungana yaani kuwa kitu kimoja, kuondoa mipaka na masafa kati ya nchi na nchi, kukusanyika pamoja na kuleta kitu kinachoitwa "kijiji-ulimwengu" [1]

Watu wana msimamo tofauti sana kuhusu suala hilo la utandawazi: baadhi wanahisi kwamba unasaidia kila mtu, wakati kuna wengine wanafikiria kwamba unaumiza baadhi ya watu. Kati ya madhara ya utandawazi katika jamii fulani kuna kuiga utamaduni wa kigeni (kwa mfano kuvaa nguo fupi) bila kufanya tathmini kwanza kama unafaa au sio.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sheila L. Croucher. Globalization and Belonging: The Politics of Identity a Changing World. Rowman & Littlefield. (2004). p.10

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Peter Berger, Four Faces of Global Culture (The National Interest, Fall 1997).
  • Friedman, Thomas L. (2005). The World Is Flat. New York: Farrar, Straus and Giroux. ISBN 0-374-29288-4. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  • Kitching, Gavin (2001). Seeking Social Justice through Globalization. Escaping a Nationalist Perspective. Penn State Press. ISBN 0-271-02162-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-28. Iliwekwa mnamo 2009-10-05. {{cite book}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  • Mander, Jerry (1996). The case against the global economy : and for a turn toward the local. San Francisco: Sierra Club Books. ISBN 0-87156-865-9. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  • Steger, Manfred (2003). Globalization: A Very Short Introduction. Oxford, New York: Oxford University Press. ISBN 0-19-280359-X. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  • Stiglitz, Joseph E. (2002). Globalization and Its Discontents. New York: W.W. Norton. ISBN 0-393-32439-7. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
  • Wolf, Martin (2004). Why Globalization Works. New Haven: Yale University Press. ISBN 978-0300102529. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utandawazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.