Nenda kwa yaliyomo

Waberberi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Watuareg)
Maeneo yenye wasemaji wa lugha za Kiberberi (Tamazight).

Waberberi ni wakazi asilia wa Afrika ya Kaskazini kuanzia Moroko hadi Misri na nchi za Sahara. Wenyewe wanajiita Amazigh (au: Imazighen) yaani "watu huru".

Kabila lao mojawapo linalojulikana hasa ni Watuareg wanaokalia maeneo ya jangwa kubwa la Sahara.

Leo hii wamepungua kwa sababu wengi wamezoea kutumia lugha ya Kiarabu, hivyo wanahesabiwa kati ya Waarabu.

Wanaoendelea kutumia lugha ya Tamazight (au: Kiberber) kama lugha ya kwanza ni:

Katika nchi kavu jangwani au karibu na jangwa maisha yao ni ya ufugaji na kuhamahama. Mlimani wanalima. Leo hii ni hasa Watuareg wanaoendelea na maisha ya kuhamahama.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia wamejulikana tangu ilipoanza kuandikwa. Waroma na Wagiriki wa Kale waliwaita kwa majina kama Wanumidia, Wagaramanti au Walibya.

Kabla ya unenezaji wa Uislamu wengi walikuwa Wakristo na mashuhuri kati hao alikuwa Monika, mama wa Agostino wa Hippo.

Mberberi anayejulikana sana leo ni mchezaji wa mpira wa Ufaransa Zinédine Zidane.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]