Hispania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wahispania)
Jump to navigation Jump to search
Reino de España
Ufalme wa Hispania
Bendera ya Hispania Nembo ya Hispania
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Plus Ultra
(Kilatini kwa "Mbele na zaidi")
Wimbo wa taifa: Marcha Real au Marcha Granadera
Lokeshen ya Hispania
Mji mkuu Madrid
40°26′ N 3°42′ W
Mji mkubwa nchini Madrid
Lugha rasmi Kihispania(1)
Serikali Ufalme wa kikatiba
Felipe VI
Mariano Rajoy
Kuungana kwa nchi
Kungana kwa ndoa za wafalme
Maungano
Hali halisi
Kisheria

1516

1716
1812
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
504,782 km² (ya 50)
1.04%
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
44.395.286 (ya 29)
40,847,371
87.8/km² (ya 106)
Fedha Euro (€)(2) (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CETKigezo:Footnote (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .es
Kodi ya simu +34

-

Kigezo:Fnb Majimbo ya kujitawala ya Hispania yanatumia lugha za: Kikatalunya/Kivalencia, Kibaski na Kigalicia pamoja na Kihispania. Katika Bonde la Val d'Aran lahaja ya Kiarani ya lugha ya Kioksitani ni lugha rasmi pamoja na Kihispania; Kigezo:Fnb Hadi 1999: Peseta
Kigezo:Fnb Ispokuwa Visiwa vya KanariHispania ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar.

Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki.

Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Hispania.

Hispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia.

Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi.

Eneo la nchi ni 500,000 km² ambalo lina wakazi wenye idadi zaidi ya watu milioni 44.395.286 (2006).

Lugha rasmi ni Kihispania lakini majimbo 17 yamepewa mamlaka ya kujitawala katika mambo mbalimbali pamoja na siasa ya kiutamaduni hivyo lugha za Kikatalunya, Kivalencia, Kibaski na Kigalicia zimekuwa lugha rasmi za kijimbo pamoja na Kihispania.

Wahispania walio wengi ni waamini wa Kanisa Katoliki.

Mfalme Felipe VI amevaa taji mwaka 2014, akishika nafasi ya baba yake Juan Carlos I, anayeheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana.

Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba, hivyo kisheria madaraka ya mfalme ni madogo.

Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya awali[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Hispania walikuwa Wakelti.

Katika karne za 1 KK Wafoinike walianzisha miji kwenye pwani na kuchimba madini hasa shaba na fedha.

Waroma[hariri | hariri chanzo]

Waroma wa Kale walivamia na kutawala Hispania kwa karne kadhaa wakileta lugha yao ya Kilatini kilichopata kuwa msingi wa lugha za kisasa za Hispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.

Katika karne ya 5 makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Hispania. Kati yao Wavandali na Wavisigothi walitawala sehemu kubwa ya Hispania.

Waarabu[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa ya Hispania hadi karibu milima ya Pirenei, lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijihami na kufaulu kudumisha uhuru wao.

Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.

Katika kipindi cha vita cha karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha nyuma Waarabu hadi kusini kwa nchi.

Hatimaye mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Granada, mji wa mwisho wa Waarabu, alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.

Makoloni ya Amerika[hariri | hariri chanzo]

Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Hispania walimkubalia nahodha Kristoforo Kolumbus kutafuta njia ya kufika Bara Hindi kupitia magharibi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.

Huo ulikuwa mwanzo wa upanuzi wa Hispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa la kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.

Katika miaka mia tatu iliyofuata Hispania ilitajirika sana kutokana na maliasili ya Amerika.

Vita vya Marekani dhidi ya Hispania[hariri | hariri chanzo]

Vita hivyo vilitokea mwaka 1898. Vilianza kwa shambulizi la Marekani tarehe 25 Aprili dhidi ya Puerto Rico vilivyokuwa koloni la Hispania na kuishia tarehe 12 Agosti 1898, jeshi la Hispania huko Manila (Ufilipino) liliposalimu amri.

Vita hivyo vilikuwa mwanzo wa Marekani kufuata siasa ya nje ya upanuzi hata katika maeneo ya mbali. Kabla ya vita hivyo Marekani ilishughulika kupanua eneo lake kwenye bara la Amerika ya Kaskazini dhidi ya wakazi asilia na dhidi ya Mexiko.

Marekani ilitumia nafasi ya ghasia ya wenyeji wa Kuba dhidi ya utawala wa kikoloni wa Hispania.

Baada ya mlipuko kwenye manowari ya Marekani USS Maine katika bandari ya Havana, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Hispania ingawa sababu ya mlipuko haijajulikana hadi leo ilikuwa nini.

Hispania haikuweza kushindana na manowari na silaha za Marekani zilizokuwa zimeendelea kiteknolojia.

Pia Marekani ilikuwa karibu na mahali pa vita na Hispania ilishindwa kuongeza wanajeshi na silaha.

Hivyo Marekani ilitwaa makoloni ya Hispania ya Puerto Rico, Kuba na Ufilipino.

(ya kuendelea)

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya Hispania

Miji mikubwa[hariri | hariri chanzo]

Picha za Hispania[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Flag of Spain.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hispania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.