Sevilla
Mandhari
(Elekezwa kutoka Sevilia)


Sevilla ni mji mkubwa kando ya mto Guadalquivir kusini mwa Hispania na mji mkuu wa jimbo la kujitawala la Andalusia.
Mwaka 2019 wakazi wake walikuwa 688,592 [1] na kuufanya wa nne nchini kwa wingi wa watu.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Mji ulianzishwa zamani za Wafinisia ukaja kukaliwa na kutawaliwa na Waroma wa Kale, Wavandali halafu na Wavisigothi na tangu mwaka 711 na Waarabu Waislamu. Mwaka 1248 ulitekwa na wafalme wa Kastilia na kubaki upande wa Hispania ya Kikristo.
Majengo mengi mazuri yanatunza kumbukumbu ya historia hiyo. Boma la Alcazar lilijengwa na mafundi Waislamu kwa niaba ya wafalme Wakatoliki. Sevilla ilikuwa na ofisi kuu ya utawala kwa makoloni ya Hispania katika Amerika.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Sevilla Guide Ilihifadhiwa 6 Februari 2008 kwenye Wayback Machine.
- Sevilla Airport
- City councils Ilihifadhiwa 12 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine. (in Kihispania only)
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Sevilla kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |