Nenda kwa yaliyomo

Guadalquivir

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Guadalquivir umepita katika mji wa Sevilla
Guadalquivir
Mto Guadalquivir mjini Cordoba
Chanzo Cañada de las Fuentes
Mdomo Bahari ya Atlantiki
Nchi Hispania
Urefu 657 km
Kimo cha chanzo 1,400 m
Tawimito upande wa kulia Genil, Gudaira
Mkondo 164.3 m³/s
Eneo la beseni 56,978 km²
Miji mikubwa kando lake Cordoba, Sevilla

Guadalquivir ni mto nchini Hispania na mto mkubwa wa Andalusia.

Jina limetokana na lugha ya Kiarabu "Wadi al-Kabir (الوادي الكبير)" yaani "mto mkubwa".

Chanzo kipo katika milima ya Sierra de Cazorla halafu mto unapita miji ya Córdoba na Sevilla ukiishia katika ghuba ya Cadiz kwenye Atlantiki.

Guadalquivir ni mto pekee wa Hispania unaopitika kwa meli za bahari wanaofika hadi Sevilla.

Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Guadalquivir kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.