Santa Cruz de Tenerife
| Jiji la Santa Cruz de Tenerife | |
| Nchi | Visiwa vya Kanari |
|---|---|
| Provincia | Tenerife |
| Idadi ya wakazi | |
| - Wakazi kwa ujumla | 207.312 |
| Tovuti: http://www.sctfe.es/ | |


Santa Cruz de Tenerife (kifupi; Santa Cruz; maana ya Kihispania: Msalaba Mtakatifu) ni makao makuu ya utawala wa kisiwa cha Tenerife na moja kati ya miji mikuu miwili ya funguvisiwa la Visiwa vya Kanari inayojitawala ndani ya Hispania. Visiwa vya Kanari vimo katika sehemu ya Kiafrika ya bahari ya Atlantiki.
Mji ulikuwa na wakazi 207.312 mwaka 2019 [1]. Uko kaskazini mwa kisiwa cha Tenerife. Bandari ni kitovu cha kihistoria cha mji. Kuna feri kati ya mji na Las Palmas de Gran Canaria.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Santa Cruz ilianzishwa mwaka 1494 Wahispania walipovamia Tenerife na kufanya vita dhidi ya wenyeji. Mahali pa mji wa sasa kiongozi Mhispania alisimamisha msalaba mkubwa wa ubao aliposheherekea ushindi juu ya Waguanche wenyeji. Mji mpya ulipokea jina kutokana na msalaba huo.
Mji ulikua kama kituo muhimu cha safari za kuvuka Atlantiki kati ya Ulaya na Amerika.
Santa Cruz ilikuwa mji mkuu wa funguvisiwa mnamo 1812. Tangu 1982 ni mji mkuu pamoja na Las Palmas de Gran Canaria. Kila baada ya miaka minne mmoja kati ya miji hii miwili una nafasi ya kuwa mji mkuu.
Picha
[hariri | hariri chanzo]- Ukumbi wa Tenerife
- Kitovu cha mji wa Santa Cruz
- Mapwa ya Playa de Las Teresitas
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kihispania) Halmaushuri ya Santa Cruz de Tenerife Ilihifadhiwa 14 Januari 2007 kwenye Wayback Machine.
- (Kihispania) Robert Blake's attack
- (Kihispania) John Genings' attack
- 'Ramani na picha za ndege au angani
- Ramani za barabara: Ramani za barabara toka Mapquest, MapPoint Ilihifadhiwa 17 Novemba 2007 kwenye Wayback Machine. au Google
- Picha za Satelaiti: Google
| Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Santa Cruz de Tenerife kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |