Bendera ya Togo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Togo

Bendera ya Togo ina milia mitano ya kulala ya kijani (juu na chini) inayobadilishana na njano. Mraba mwekundu uonyeshayo nyota nyeupe ya pembe tano uko kwenye kona ya juu upande wa kushoto.

Bendera hii ni kati bendera zinazotumia rangi za Umoja wa Afrika. Rangi za kijani, njano na nyekundu huitwa rangi za umoja wa Afrika kwa sababu zinapatikana kwenye bendera ya Ethiopia, nchi ya pekee iliyofaulu kujitetea dhidi ya dhidi ya uvamizi wa kikoloni katika karne ya 19 BK.

Pamoja na kutumia rangi za Ethiopia bendera ya Togo imefanana na tarakibu ya bendera ya Liberia ambayo ni nchi ya pili ya Afrika isiyokuwa koloni. Tarakibu hii ni karibu na bendera ya Marekani ambayo ni nchi walipotoka waanzilishaji wa nchi ya Liberia.

Bendera imeonyeshwa rasmi mara ya kwanza tarehe 27. Aprili 1960.