Rangi za Umoja wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bendera ya Ethiopia yenye rangi tatu za kijani, njano na nyekundu

Rangi tatu kijani, njano na nyekundu huitwa rangi za umoja wa Afrika kwa sababu zinapatikana kwenye bendera ya Ethiopia, nchi ya pekee ya Afrika iliyofaulu kujitetea dhidi ya dhidi ya uvamizi wa kikoloni katika karne ya 19 BK.

Tangu kuenea kwa uhuru kwenye nchi za Afrika katika miaka ya 1950 na 1960 kuna nchi mbalimbali zilizochagua rangi zilezile kwa kuonyesha upendeleo wao kwa umoja wa Afrika. Ghana ilikuwa nchi ya kwanza ya kutoka katika ukoloni mwaka 1957 ikateua rangi za Ethiopia kwa bendera yake.

Bendera za nchi zifuatazo hutumia rangi za Ethiopia ama pekee au pamoja na rangi nyingine. Mara nyingi ni nyeusi kama alama ya watu weusi.

Bendera za nchi kadhaa za Amerika zinatumia rangi zilezile kwa sababu wakazi wao ni watoto wa watumwa kutoka Afrika.

Nchi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Nchi za Amerika ya Kusini na Karibi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]