Bendera ya Guinea-Bissau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Guinea-Bissau

Bendera ya Guinea-Bissau ina milia mitatu ya rangi nyekundu, njano na kijani pamoja na nyota nyeusi. Mlia mwekundu ulio na nyota nyeusi unasimama upande wa nguzo lakini mbili za njano na kijani zimelala. Hizi ni rangi za bendera ya Ethiopia au rangi za Umoja wa Afrika.

Bendera hii imekuwa bendera rasmi tangu mwaka 1973 nchi ilipopata uhuru kutoka Ureno.