Bendera ya Algeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Algeria

Bendera ya Algeria ina milia miwili ya kusimama ya upana uleule. Kushoto rangi ni kijani na upande wa kulia nyeupe. Katikati kuna hilali nyekundu au mwezi mwandamo mwekundu pamoja na nyota ya pembetano nyekundu.

Nyeupe inatakiwa kumaanisha usafi na rangi ya kijani humaanisha Uislamu. Hilali na nyota ni sehemu za nembo au bendera katika nchi nyingi za kiislamu tangu bendera ya Dola la Uturuki.

Bendera hii ilikubaliwa wakati wa uhuru tarehe 3. Julai 1962. Inafanana na bendera za zamani ya Chama cha Ukombozi wa Kitaifa (FLN).