Bendera ya Jibuti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Flag ratio: 4:7

‘’’Bendera ya Taifa la Jiibuti’’’ ina mistari miwili ikatayo kushoto hadi kulia, rangi ya Samawati (juu) na Kijani ikiwa na umbo la Pembe tatu la rangi Nyeupe ikikalia sehemu ya kuinulia, ikiwa na nyota ya sehamu tano ya rangi Nyekundu (ikiashiria sehemu tano Wasomali waishiko katika eneo hilo) katikati. Sehemu hizi tano ni British somaliland (Somalia), Italian Somaliland (Somalia), French Somaliland (Jibuti), Ogaden na Mkoa wa Kaskazini Mashariki (Kenya).

Maana ya Rangi zilizotumika[hariri | hariri chanzo]

Rangi zilizoyumuwa zinaweza kuashiria Ardhi (Kijani), Bahari na Anga (Samawati) pamoja na Amani Nyeupe. Nyota nyekundu inaashiria umoja.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Bendera hii ilipandishwa mara ya kwanza mnamo 27 Juni 1977 wakati wa Uhuru wa Jibuti. Bendera ya Taifa ambayo iliundwa wakati wa Uhuru mnamo 1977 ilikuwa ikifanana na bendera ya Ligue Populaire Africaine pour l'Independence (LPAI) ambayo iliiongoza nchi hiyo kupata uhuru. Bendera ya LPAI ilikuwa na umbo la Pembe Tatu jekundu na nyota nyeupe. Kwa bendera ya Taifa, nyota hii iliwekwa kutazama juu badala ya kuegemea upande mmoja. Pia sehemu zote za bendera zilirefushwa kwa usawa. Rangi ya Samawati ambayo haijakolea inawaashiria watu wa ukoo wa Issa wa Somali na Kijani inawakilisha watu wa Afar. Nyeupe, Kijani na samawati isiyokolea ndizo rangi za LPAI. Nyota nyekundu inaashiria umoja wa taifa lililo na watu wa makabila mbalimbali.


Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]