Bendera ya Senegal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bendera ya Senegal

Bendera ya Senegal ina milia tatu za wima pamoja na nyota ya pembetatu katikati.

Milia ni ya nyekundu, njano na kijani kibichi. Nyota ni ya kijani.

Maana ya rangi ni kama zifuatazo:

  • Nyekundu hudokeza kwa mapambano ya uhuru, damu iliyomwagika na matumaini ya ujamaa
  • Njano ni rangi ya dhahabu na utajiri unaotokana na kazi ya pamoja
  • kijani ni rangi ya tumaini na maendeleo pia hukumbusha dini ya wa raia wengi ambayo ni Uislamu.

Asili ni bendera ya Shirikisho ya Mali ya 1959. Wakati ule Senegal na Sudan ya Kifaransa zilikuwa pamoja katika Shirikisho ya Mali hadi 1960. Bendera ya shirikisho ilikuwa ileile isipokuwa ilionyesha umbo nyeusi ya mwanadamu katikati. Senegal iliandelea na bendera lakini umbo la mtu lilibadilishwa kwa nyota.

Rangi ni zilezile zinazopatikana katika bendera nyingi za kiafrika kutokana na athari ya Ethiopia kama nchi ya Afrika iliyofaulu kujitetea dhidi majaribio ya kuitawala kikoloni.