Bendera ya Mali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Mali
Bendera ya Shirikisho la Mali hadi Machi 1961

Bendera ya Mali ina milia mitatu ya wima ya rangi nyekundu, njano na kijani kibichi. Rangi hizi ambazo huitwa rangi za Umoja wa Afrika ni zilezile zinazopatikana katika bendera nyingi za nchi za Afrika kutokana na athari ya Ethiopia kama nchi ya Afrika iliyofaulu kujitetea dhidi majaribio ya kuitawala kikoloni.


Maana ya rangi ni kama zifuatazo:

  • Nyekundu hudokeza kwa mapambano ya uhuru, damu iliyomwagika na matumaini ya ujamaa
  • Njano ni rangi ya dhahabu na utajiri unaotokana na kazi ya pamoja
  • Kijani ni rangi ya tumaini na maendeleo pia hukumbusha dini ya wa raia wengi ambayo ni Uislamu.

Bendera hii imetumiwa tangu uhuru wa kitaifa mwaka 1961.

Nchi ilipata uhuru ngazi ya kwanza yaani madaraka ya kujitawala mwaka 1959. Wakati ule ilikuwa imeungana na Senegal kama "Shirikisho la Mali". Bendera ile ya kwanza ilionyesha umbo la mwanadamu. Mali ilipobaki peke yake ilifuta picha kwa sababu ya kanuni za imani ya Kiislamu zinazokataza picha ya watu.

Senegal iliendelea na bendera ileile isipokuwa ina nyota ya kijani katika mlia wa katikati.