Bendera ya Zimbabwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Zimbabwe

Bendera ya Zimbabwe ni ya milia saba ya kulala na pembetatu upande wa nguzo.

Rangi za milia ni kimsingi ile ya Ethiopia au rangi za Umoja wa Afrika: kijani - njano - nyekundu. Rangi hizo zinarudia mara mbili lakini ufuatano unabadilishwa. Mlia wa saba katikati ni nyeusi.

Rangi hizo zilipatikana pia kwenye bendera ya chama cha ZANU.

Milia ya tatu ya juu ni sawa kabisa na bendera ya Ethiopia.

Milia mitatu ya chini ni sawa kabisa na bendera ya Ghana inayofuata kielelezo cha Ethiopia lakini kwa kubadilisha ufuatano wa rangi.

Hivyo bendera inaunganisha bendera ya nchi ya Afrika iliyofaulu kujitetea dhidi ya ukoloni na bendera ya kwanza katika Afrika iliyopata uhuru baada ya ukoloni.

Mlia mweusi wa katikati inadokeza rangi ya kawaida ya watu wa Afrika.

Pembetatu nyeupe upande wa nguzo inaonyesha picha ya ndege juu ya nyota nyekundu.

Ndege ni mfano wa sanamu za ndege wa jiwe la steatiti zilizopatikana katika maghofu ya Zimbabwe Kuu. Imekuwa nembo la nchi.

Nyota nyekundu chini yake hukumbusha mapambano ya ukombozi.