Waewe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Waewe (Éwé) ni kabila kubwa la Togo na Ghana ya kusini.

Lugha yao ni Kiewe (Eʋegbe. Jina la lugha limeandikwa au kuitwa pia: Eibe, Ebwe, Eve, Efe, Eue, Vhe, Gbe, Krepi, Krepe, au Popo.)

Kwa jumla kuna takriban wasemaji 3,300,000. Kati yao wako 2,250,000 Ghana (2003) na 860,000 Togo (1991).

Lugha yao hufundishwa katika shule za msingi, Ghana hata katika shule za sekondari.

Katika Togo ni lugha ya taifa na lugha ya kwanza ya mawasiliano ya Togo Kusini.

Waewe wanasemekana wametokea Nigeria. Utaratibu wa kijamii hufuata baba.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waewe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.