Kakao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mbegu za kakao ndani ya mkokwa
Unga wa kakao ni msingi wa kutengeneza kinywaji na pia chokoleti

Kakao (pia: kakau[1]; kwa Kiingereza: cocoa) ni zao la mkakao linalotolewa kutoka mbegu katika tunda linaloitwa mkokwa.

Jina hilo hutumiwa kwa ajili ya mbegu za mkakao, unga unaotengenezwa kutoka mbegu hizo na pia kinywaji kinachotengenezwa kwa unga wa mbegu pamoja na maji, maziwa na sukari.

Matumizi ya kakao yalianza pale Amerika ya Kati, hasa Meksiko ambako walipenda kinywaji lakini walitumia pia mbegu kama pesa[2].

Mbegu ya kakao huvunjwa, hukaangwa na kusagwa; kuna mafuta mengi ndani ya mbegu, na kwa matumizi ya kinywaji ni lazima kutenganisha mafuta na unga kavu; hivyo sehemu kubwa ya mafuta ya kakao hutolewa; kwa chokoleti yanahitajika tena[3].

Mkakao hulimwa sana nchini Ghana, lakini pia Tanzania maeneo kama vile Kyela.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kakau ni tahajia inayopendezwa zaidi na kamusi ya KKS
  2. Pushing back the origin of chocolate, tovuti ya .natureasia.com, iliangaliwa Oktoba 2020
  3. Zipperer, Paul (1902). The manufacture of chocolate and other cacao preparations (3rd ed.). Berlin: Verlag von M. Krayn, inapatikana archive.org
Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kakao kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.