Wanuba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu eneo katika kaskazini ya Sudan, tazama Nubia

Mwanamke Mnuba

Wanuba ni makabila mbalimbali ya watu ambao wanaishi katika Milima ya Nuba kwenye jimbo la Kordofan Kusini nchini Sudan, karibu na mpaka wa Sudan Kusini. Wanuba wanajumuisha watu tofautitofauti wanaozungumza lugha tofauti. Makadirio ya idadi ya watu wanaoitwa Wanuba yanatofautiana sana; serikali ya Sudan ilikadiria kuwa walifikia milioni 2.07 mwaka wa 2003. [1] Milima ya Nuba katika Southern Kordofan, Sudan. Jina "Wanuba" lisichanganywe na "Wanubia" wa kaskazini mwa Sudan na kusini mwa Misri. [2]

Takriban asilimia 90 ya wakazi wa eneo la Milima ya Nuba ni Waafrika Weusi ambao ni wakulima wanaofuga pia. Watu wa Nuba wanaishi katika mojawapo ya maeneo ya mbali na yasiyofikika ya Sudan, chini ya Milima ya Nuba kwenye kusini ya Sudan. Eneo hilo la milima lilikuwa mahali pa kimbilio, likipokea watu wa lugha na malezi mbalimbali waliokuwa wakikimbia serikali dhalimu na wafanyabiashara ya utumwa. Idadi ya makabila ni takriban 50 wenye lugha zao zinazojumuishwa katika makundi 10 ya lugha. Asilimia 10 ya wakazi wa eneo ni wafugaji Waarabu wanaoitwa Wabaggara, pamoja na wafanyabiashara wachache Waarabu.

Wanuba wengi huzungumza pia Kiarabu cha Sudan, lugha ya kawaida ya Sudan.

Dini kuu ya Wanuba ni Uislamu, ila baadhi yao ni Wakristo, na dini za jadi zina wafuasi pia. [3]

Vita katika Milima ya Nuba[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Sudan na kabla ya ugawaji wa nchi, vikosi vya SPLA vilipigania katika Milima ya Nuba. Katika mapatano ya amani ya mwaka 2005, maeneo ya Kordofan Kusini (pamoja na Milima ya Nuba), Abyei na Nile Buluu yalibaki kwa muda kama sehemu za Sudan kura ya wakazi zilizotakiwa kutekelezwa hadi mwaka 2011 lakini kutokana na siasa ya Sudan hadi leo hazikufanywa.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. South Kordofan
  2. Winter, Roger (2000), Spaulding, Jay, ed., "The Nuba People: Confronting Cultural Liquidation", White Nile Black Blood: War, Leadership, and Ethnicity from Khartoum to Kampala (Lawrenceville, NJ: The Red Sea Press), archived from the original on 2000-04-09 
  3. Sudan: Nuba. Miniority Rights Group. Jalada kutoka ya awali juu ya 2021-12-11. Iliwekwa mnamo 2021-12-11. “Some traditional religions survive but most Nuba have been converted to Islam or Christianity.”

Kujisomea zaidi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]